Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.
Methali 11:13 - Swahili Revised Union Version Mwenye udaku hupitapita akifunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Apitapitaye akichongea hutoa siri, lakini anayeaminika rohoni huficha siri. Biblia Habari Njema - BHND Apitapitaye akichongea hutoa siri, lakini anayeaminika rohoni huficha siri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Apitapitaye akichongea hutoa siri, lakini anayeaminika rohoni huficha siri. Neno: Bibilia Takatifu Masengenyo husaliti uaminifu, bali mtu mwaminifu hutunza siri. Neno: Maandiko Matakatifu Masengenyo husaliti tumaini, bali mtu mwaminifu hutunza siri. BIBLIA KISWAHILI Mwenye udaku hupitapita akifunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo. |
Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.
Ndipo wakuu wakamwendea Yeremia, wakamwuliza; naye akawaambia sawasawa na maneno aliyoamriwa na mfalme. Basi wakaacha kunena naye; maana neno lile halikujulikana.
Usiende huku na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usijifaidi kwa damu ya jirani yako; mimi ndimi BWANA.
Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizungukazunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa.
Wale wanaume wakamwambia, Tutautoa uhai wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari ya shughuli yetu hii; kisha itakuwa, wakati BWANA atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa hisani na uaminifu.
Lakini wewe ukitangaza habari yetu hii, ndipo tutakuwa hatuna hatia, katika kiapo hiki ulichotuapisha.