Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 19:16 - Swahili Revised Union Version

16 Usiende huku na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usijifaidi kwa damu ya jirani yako; mimi ndimi BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Kamwe usipitepite ukiwachongea watu wa jamaa yako. Usiyatie maisha ya jirani yako katika hatari ya kifo kwa maneno yako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Kamwe usipitepite ukiwachongea watu wa jamaa yako. Usiyatie maisha ya jirani yako katika hatari ya kifo kwa maneno yako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Kamwe usipitepite ukiwachongea watu wa jamaa yako. Usiyatie maisha ya jirani yako katika hatari ya kifo kwa maneno yako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 “ ‘Usieneze uchochezi miongoni mwa watu wako. “ ‘Usifanye kitu chochote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 “ ‘Usieneze uchochezi miongoni mwa watu wako. “ ‘Usifanye kitu chochote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimi bwana.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Usiende huku na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usijifaidishe kwa damu ya jirani yako; mimi ndimi BWANA.

Tazama sura Nakili




Walawi 19:16
24 Marejeleo ya Msalaba  

Awafitiniye rafiki zake wawe mawindo, Hata macho ya watoto wake yataingia kiwi.


Amsingiziaye jirani yake kwa siri, Huyo nitamwangamiza. Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, Huyo sitamvumilia.


Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala kumtenda mwenziwe mabaya, Wala kumsengenya jirani yake.


Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia.


Usimshuhudie jirani yako uongo.


Usivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo.


Jitenge mbali na neno la uongo; wala wasio hatia na wenye haki usiwaue; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu.


Yeye afichaye chuki ana midomo ya uongo, Na yeye asingiziaye ni mpumbavu.


Mwenye udaku hupitapita akifunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.


Mwenye udaku hufunua siri; Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana.


Ni waasi kupita kiasi wote pia, waendao huku na huko wakisingizia, ni shaba na chuma hao, hutenda dhuluma wote pia.


Jihadharini, kila mtu na jirani yake, wala msimtumaini ndugu awaye yote; maana kila ndugu atachongea, na kila jirani atakwenda huku na huko na kusingizia.


Wasingiziaji wamekuwamo ndani yako, ili kumwaga damu; na ndani yako wamekula juu ya milima; kati yako wamefanya uasherati.


Wakasema, Basi, haya yatuhusu nini sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.


Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Amina.


Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; wasiwe wachongezi; ila wawe watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.


wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,


Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wanaofundisha yaliyo mema;


Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.


Tazama, leo hivi macho yako yameona jinsi BWANA alivyokutia mikononi mwangu pangoni, na watu wengine wakaniambia nikuue; lakini nikakuacha; nikasema, Sitaki kuunyosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo