Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 19:15 - Swahili Revised Union Version

15 Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 “Unapotoa hukumu uamue kwa haki; usimpendelee maskini wala kumwogopa mwenye cheo. Bali ni lazima kumwamua jirani kwa haki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 “Unapotoa hukumu uamue kwa haki; usimpendelee maskini wala kumwogopa mwenye cheo. Bali ni lazima kumwamua jirani kwa haki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 “Unapotoa hukumu uamue kwa haki; usimpendelee maskini wala kumwogopa mwenye cheo. Bali ni lazima kumwamua jirani kwa haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 “ ‘Usipotoshe haki; usioneshe kumpendelea maskini, wala upendeleo kwa mwenye cheo, bali mwamulie jirani yako kwa haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 “ ‘Usipotoshe haki; usionyeshe kumpendelea maskini, wala upendeleo kwa mwenye cheo, bali mwamulie jirani yako kwa haki.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.

Tazama sura Nakili




Walawi 19:15
20 Marejeleo ya Msalaba  

Je! Mtamwonesha yeye upendeleo? Mtamtetea Mungu?


Tafadhali, nisiupendelee uso wa mtu; Wala sitajipendekeza kwa mtu yeyote.


Sembuse yeye huwajali nyuso za wakuu, Wala hawajali matajiri kuliko maskini? Kwani wote ni kazi ya mikono yake,


Hadi lini mtahukumu kwa dhuluma, Na kuzikubali nyuso za wabaya?


Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mamia, na wakuu wa hamsini hamsini, na wakuu wa kumi kumi;


Kukubali uso wake asiye haki si vizuri; Wala kumpotosha mwenye haki hukumuni.


Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili. Kupendelea watu katika hukumu si kwema.


Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; Uwapatie maskini na wahitaji haki yao.


Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo.


Basi msihukumu kwa kuangalia kwa nje tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.


Ndipo Paulo akamwambia, Mungu atakupiga wewe, ukuta uliopakwa chokaa. Wewe umeketi kunihukumu kulingana na sheria, nawe unaamuru nipigwe kinyume cha sheria?


Msitazame nafsi za watu katika hukumu; muwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu yeyote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza.


Kwa maana BWANA, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea watu, wala kukubali rushwa.


Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza kesi wa wenye haki.


Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo