Msiwe kama farasi wala nyumbu, Wasiokuwa na akili. Kwa matandiko ya lijamu na hatamu Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia.
Methali 10:13 - Swahili Revised Union Version Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu; Bali fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kinywani mwa mwenye ufahamu mna hekima, lakini wasio na akili watachapwa viboko mgongoni. Biblia Habari Njema - BHND Kinywani mwa mwenye ufahamu mna hekima, lakini wasio na akili watachapwa viboko mgongoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kinywani mwa mwenye ufahamu mna hekima, lakini wasio na akili watachapwa viboko mgongoni. Neno: Bibilia Takatifu Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua, lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu. Neno: Maandiko Matakatifu Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua, lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu. BIBLIA KISWAHILI Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu; Bali fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu. |
Msiwe kama farasi wala nyumbu, Wasiokuwa na akili. Kwa matandiko ya lijamu na hatamu Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia.
BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya nchi ya Misri kwa hao nzige, ili wakwee juu ya nchi ya Misri, waile mimea yote ya nchi, yaani, vyote vilivyosazwa na ile mvua ya mawe.
Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini!
Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng'ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;
Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.
Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu?