Luka 14:11 - Swahili Revised Union Version Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa maana yeyote anayejikweza atashushwa na anayejishusha, atakwezwa.” Biblia Habari Njema - BHND Kwa maana yeyote anayejikweza atashushwa na anayejishusha, atakwezwa.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa maana yeyote anayejikweza atashushwa na anayejishusha, atakwezwa.” Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana kila mtu ajikwezaye atashushwa, naye ajishushaye atakwezwa.” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana kila mtu ajikwezaye atashushwa, naye ajishushaye atakwezwa.” BIBLIA KISWAHILI Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. |
Basi mfalme akamwambia Hamani, Hima! Twaa mavazi na farasi kama ulivyosema, ukamfanyie vivyo hivyo Mordekai, Myahudi, aketiye mlangoni pa mfalme; lisipungue neno lolote katika yote uliyoyasema.
Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.
Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.
Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu kitashushwa; naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika nawe ukapata malipo.
Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha makabila ya Israeli? Naye BWANA akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli.