Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Samueli 15:17 - Swahili Revised Union Version

17 Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha makabila ya Israeli? Naye BWANA akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Samueli akamwambia, “Ingawa unajiona kuwa wewe si maarufu, je, wewe si kiongozi wa makabila ya Israeli? Mwenyezi-Mungu alikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Samueli akamwambia, “Ingawa unajiona kuwa wewe si maarufu, je, wewe si kiongozi wa makabila ya Israeli? Mwenyezi-Mungu alikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Samueli akamwambia, “Ingawa unajiona kuwa wewe si maarufu, je, wewe si kiongozi wa makabila ya Israeli? Mwenyezi-Mungu alikupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Samweli akamwambia, “Ingawa zamani ulijiona mdogo machoni pako mwenyewe, Je, hukuwa kiongozi wa makabila ya Israeli? Mwenyezi Mungu alikupaka mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Samweli akamwambia, “Ingawa zamani ulijiona mdogo machoni pako mwenyewe, Je, hukuwa kiongozi wa kabila za Israeli? bwana alikutia mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

17 Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha makabila ya Israeli? Naye BWANA akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli.

Tazama sura Nakili

1 Samueli 15:17
8 Marejeleo ya Msalaba  

Efraimu aliponena, palikuwa na tetemeko; alijitukuza katika Israeli; Lakini alipokosa katika Baali, alikufa.

Basi, yeyote ajinyenyekezaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.

Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu.

Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! BWANA hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa kutoka kwa mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake.

Basi wakazidi kumwuliza BWANA, Amebaki mtu asiyekuja huku bado? Naye BWANA akajibu, Tazama, amejificha kwenye mizigo.

Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia BWANA usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema.

Basi Sauli akajibu, akasema, Je! Mimi si Mbenyamini, mtu wa kabila iliyo ndogo kuliko kabila zote za Israeli? Na jamaa yangu nayo si ndogo kuliko jamaa zote za kabila la Benyamini? Kwa nini basi, kuniambia hivyo?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo