Rafiki, unajua inatia moyo sana kujua kwamba hata katikati ya changamoto za maisha, tunao uwezo wa Mungu ndani yetu. Kama mtoto wa Mungu, hutawahi kuwa peke yako katika hali yoyote ile. Mungu yupo pamoja nawe daima. Yeye hutangulia mbele yako akipigana vita zako na kukupa nguvu zake ili upate ushindi katika hali unayopitia.
Katika 2 Wakorintho 12:9-10, Mungu anasema kwamba neema yake inakutosha kwa sababu uweza wake unakamilika katika udhaifu wako. Ni jambo la ajabu kujua kwamba katikati ya hayo unayopitia, matatizo yako, udhaifu wako, Mungu yupo hapo akikamilisha uweza wake katika maisha yako.
Mungu anatuvika nguvu zake. Katika Luka 24:49 inasema, "Tazama, nitawatumia juu yenu yeye aliyeahidiwa na Baba yangu; lakini ninyi kaeni mjini Yerusalemu hata mvikwe nguvu kutoka juu." Tuna Mungu mweza yote, ambaye kwake hakuna lisilowezekana. Anaweza kufanya lolote. Mtumainie yeye naye atatenda katika maisha yako.
Mpendeni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa moyo wenu wote, kwa roho yenu yote na kwa nguvu zenu zote.
Yesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote’.
Kisha kutoka humohumo nchini mtamtafuta Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nanyi mtampata kama mkimtafuta kwa moyo wote na roho yote.
Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu na ngao yangu; tegemeo la moyo wangu limo kwake. Amenisaidia nami nikashangilia kwa moyo; kwa wimbo wangu ninamshukuru.
tambiko yangu kwako ee Mungu, ni moyo mnyofu; wewe, ee Mungu, hukatai moyo mnyofu na mtiifu.
Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu; wewe wanijua kabisakabisa.
Lakini wakati waja, tena umekwisha wasili, ambapo wenye kuabudu wa kweli watamwabudu Baba katika roho na ukweli. Maana Baba anawataka watu wanaomwabudu namna hiyo.
Mungu ni roho, na watu wanaomwabudu lazima wamwabudu kwa Roho na ukweli.”
Enyi watu, mtumainieni Mungu daima; mfungulieni Bwana yaliyo moyoni mwenu. Mungu ndiye kimbilio la usalama wetu.
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Nitamshukuru Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote, nikijumuika na jamii ya watu waadilifu.
Mimi nitakusifu wala sitakaa kimya. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu nitakushukuru milele.
Basi, nyinyi mcheni Mwenyezi-Mungu na kumtumikia kwa uaminifu kwa moyo wenu wote. Kumbukeni yale mambo makuu aliyowatendea.
Kila mfanyacho, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu.
Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lile alilowawekea watu wake. Mtumikieni Kristo Bwana!
Nitamwimbia Mwenyezi-Mungu maisha yangu yote; nitamsifu Mungu wangu muda wote niishipo.
Nitawapeni moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu. Nitauondoa kwenu moyo mgumu kama jiwe na kuwapa moyo wa utii.
kutimiza matakwa yako, ee Mungu wangu ni furaha yangu, sheria yako naishika kwa moyo wangu wote!”
Lakini mimi nitaimba sifa za nguvu yako; nitashangilia asubuhi juu ya fadhili zako; maana wewe umekuwa ngome yangu na kimbilio langu wakati wa taabu.
Mpeni Mwenyezi-Mungu heshima ya utukufu wa jina lake; leteni tambiko na kuingia nyumbani mwake. Mwabuduni Mwenyezi-Mungu patakatifuni pake.
Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungu tambiko ya sifa daima, yaani sifa zinazotolewa kwa midomo inayoliungama jina lake.
Kwa hiyo, ndugu zangu, maadamu Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: Mtoleeni Mungu miili yenu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu.
Furahini kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu enyi waadilifu; mshukuruni kwa ajili ya jina lake takatifu.
Bwana asema, “Watu hawa huja kuniabudu kwa maneno matupu, hali mioyo yao iko mbali nami. Wananiheshimu kulingana na mapokeo ya watu tu, jambo walilojifunza wao wenyewe.
“Sasa, enyi Waisraeli, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anataka nini kwenu, ila kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuzifuata njia zake zote, kumpenda, kumtumikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na kwa roho zenu zote,
na kuzitii amri na masharti ya Mwenyezi-Mungu ninayowawekea leo, kwa manufaa yenu wenyewe?
“Haya! Twende nyumbani kwa Mungu, tuabudu mbele ya kiti chake cha enzi!”
Inuka ee Mwenyezi-Mungu, nenda kwenye maskani yako; inuka pamoja na sanduku la agano la uwezo wako!
Makuhani wako wawe waadilifu daima; na waaminifu wako wapige vigelegele vya furaha!
Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe.
Umtambue Mungu katika kila ufanyalo, naye atazinyosha njia zako.
Msiwe na wasiwasi juu ya kitu chochote, ila kwa kila hali, mwombeni Mungu katika sala juu ya mahitaji yenu, kwa shukrani.
Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote za watu italinda salama mioyo na akili zenu katika kuungana na Kristo Yesu.
Lakini nyinyi ni ukoo mteule, makuhani wa Mfalme, taifa takatifu; watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani, akawaingizeni katika mwanga wake mkuu.
Ndipo watu wakafurahi kwa sababu walitoa kwa hiari, maana kwa moyo wao wote walimtolea Mwenyezi-Mungu kwa hiari, naye mfalme Daudi alifurahi sana.
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Umsifu Mwenyezi-Mungu, ee nafsi yangu!
Mwenyezi-Mungu atawala milele, Mungu wako, ee Siyoni, ni mfalme vizazi vyote! Msifuni Mwenyezi-Mungu!
Nitamsifu Mwenyezi-Mungu maisha yangu yote; nitamwimbia Mungu wangu muda wote niishipo.
Mkaribieni Mungu, naye atakuja karibu nanyi. Osheni mikono yenu enyi wakosefu! Safisheni mioyo yenu enyi wanafiki!
ili nao watu wa mataifa mengine wapate kumtukuza Mungu kwa sababu ya huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Kwa hiyo nitakusifu miongoni mwa watu wa mataifa. Nitaziimba sifa za jina lako.”
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Jinsi gani ilivyo vizuri kumwimbia sifa Mungu wetu! Yeye ni mwema na astahili kuimbiwa sifa.
Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na Zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu.
ya kuwa mtumishi wa Yesu Kristo kwa watu wa mataifa. Ni jukumu langu la kikuhani kuihubiri Habari Njema ya Mungu ili watu wa mataifa mengine wapate kuwa tambiko inayokubaliwa na Mungu, tambiko iliyotakaswa na Roho Mtakatifu.
Watu waliotahiriwa kikweli ni sisi, si wao; kwani sisi twamwabudu Mungu kwa njia ya Roho wake, na kuona fahari katika kuungana na Kristo Yesu. Mambo ya nje tu hatuyathamini.
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya; msifuni katika kusanyiko la waaminifu!
Najitahidi kukutii kwa moyo wote; usiniache nikiuke amri zako.
Nawapita wazee kwa busara yangu, kwa sababu nazishika kanuni zako.
Najizuia nisifuate njia mbaya, nipate kulizingatia neno lako.
Sikukiuka maagizo yako, maana wewe mwenyewe ulinifundisha.
Maneno yako ni matamu sana kwangu; naam, ni matamu kuliko asali!
Kwa kanuni zako napata hekima, kwa hiyo nachukia kila mwenendo mbaya.
Neno lako ni taa ya kuniongoza, na mwanga katika njia yangu.
Nimeapa na kuthibitisha kiapo changu, kwamba nitashika maagizo yako adili.
Ee Mwenyezi-Mungu, ninateseka mno; unijalie uhai kama ulivyoahidi.
Ee Mwenyezi-Mungu, upokee sala yangu ya shukrani; na kunifundisha maagizo yako.
Maisha yangu yamo hatarini daima, lakini siisahau sheria yako.
Nimeshika neno lako moyoni mwangu, nisije nikakukosea.
Alinifundisha wimbo mpya, wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, na kumtumainia Mwenyezi-Mungu.
‘Mungu asema: Watu hawa huniheshimu kwa maneno tu, lakini mioyoni mwao wako mbali nami.
Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu.’”
Kila mmoja, basi, na atoe kadiri alivyoamua, kwa moyo na wala si kwa huzuni au kwa kulazimishwa, maana Mungu humpenda yule mwenye kutoa kwa furaha.
Tutashangilia kwa ajili ya ushindi wako; tutatweka bendera kulitukuza jina la Mungu wetu. Mwenyezi-Mungu akutimizie maombi yako yote!
Kama paa atamanivyo maji ya kijito, ndivyo ninavyokutamani, ee Mungu wangu!
Nimepondwa kwa matukano yao, wanaponiuliza kila siku: “Yuko wapi, Mungu wako!”
Mbona nasononeka hivyo moyoni? Kwa nini nahangaika hivyo? Nitamtumainia Mungu, maana nitamsifu tena Mungu, aliye msaada wangu na Mungu wangu.
Naona kiu ya Mungu, kiu ya Mungu aliye hai. Nitafika lini kwake na kuuona uso wake?