Methali 8:35 - Swahili Revised Union Version Maana yeye anionaye mimi aona uzima, Naye atapata kibali kwa BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayenipata mimi amepata uhai, amepata upendeleo kwa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Anayenipata mimi amepata uhai, amepata upendeleo kwa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayenipata mimi amepata uhai, amepata upendeleo kwa Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana yeyote anipataye mimi amepata uzima, na kujipatia kibali kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana yeyote anipataye mimi amepata uzima, na kujipatia kibali kutoka kwa bwana. BIBLIA KISWAHILI Maana yeye anionaye mimi aona uzima, Naye atapata kibali kwa BWANA. |
Kwa maana ulinzi wa hekima ni kama ulinzi wa fedha na ubora wa maarifa ni kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Amwaminiye Mwana ana uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;