Methali 8:21 - Swahili Revised Union Version Niwarithishe mali wale wanipendao, Tena nipate kuzijaza hazina zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi huwatajirisha wanaonipenda, huzijaza tele hazina zao wanipendao. Biblia Habari Njema - BHND Mimi huwatajirisha wanaonipenda, huzijaza tele hazina zao wanipendao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi huwatajirisha wanaonipenda, huzijaza tele hazina zao wanipendao. Neno: Bibilia Takatifu nawapa utajiri wale wanaonipenda na kuzijaza hazina zao. Neno: Maandiko Matakatifu nawapa utajiri wale wanipendao na kuzijaza hazina zao. BIBLIA KISWAHILI Niwarithishe mali wale wanipendao, Tena nipate kuzijaza hazina zao. |
Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kulia Mna mema ya milele.
Kuna hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima; Bali mwanadamu aliye mpumbavu huyameza.
Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang'anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo.
tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu.
Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.