Kwa kuwa umekuja jana tu kwa nini nikusumbue leo, na kukuzungusha huku na huko pamoja nasi nami hapa ninaenda niwezapo kwenda? Rudi wewe, ukawarudishe na ndugu zako; rehema na kweli ziwe pamoja nawe.
Methali 3:3 - Swahili Revised Union Version Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utii na uaminifu visitengane nawe. Vifunge shingoni mwako; viandike moyoni mwako. Biblia Habari Njema - BHND Utii na uaminifu visitengane nawe. Vifunge shingoni mwako; viandike moyoni mwako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utii na uaminifu visitengane nawe. Vifunge shingoni mwako; viandike moyoni mwako. Neno: Bibilia Takatifu Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe; vifunge shingoni mwako, viandike katika ubao wa moyo wako. Neno: Maandiko Matakatifu Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe; vifunge shingoni mwako, viandike katika ubao wa moyo wako. BIBLIA KISWAHILI Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. |
Kwa kuwa umekuja jana tu kwa nini nikusumbue leo, na kukuzungusha huku na huko pamoja nasi nami hapa ninaenda niwezapo kwenda? Rudi wewe, ukawarudishe na ndugu zako; rehema na kweli ziwe pamoja nawe.
Nayo itakuwa ishara kwako katika mkono wako, na kwa ukumbusho kati ya macho yako, ili kwamba sheria ya BWANA ipate kuwa kinywani mwako; kwani BWANA alikuondoa utoke Misri kwa mkono wenye uwezo.
BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;
Fadhili na uaminifu humhifadhi mfalme, Na kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa fadhili.
Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma, na kwa ncha ya almasi; imechorwa katika kibao cha moyo wao, na katika pembe za madhabahu zenu;
Lisikieni neno la BWANA, enyi wana wa Israeli; kwa maana BWANA ana shutuma nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.
Sheria ya kweli ilikuwa kinywani mwake, wala udhalimu haukuonekana midomoni mwake; alikwenda pamoja nami katika amani na unyofu, na kuwageuza wengi hata wakaacha uovu.
Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa, bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.
mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoiandaa, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.
Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika fikira zao nitaziandika; ndipo anenapo,