Nawe ukienda katika njia zangu, na kuyashika mausia yangu, na amri zangu, kama baba yako Daudi alivyokwenda, basi nitazifanya siku zako kuwa nyingi.
Methali 3:2 - Swahili Revised Union Version Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana yatakupa wingi wa siku, maisha marefu na fanaka kwa wingi. Biblia Habari Njema - BHND Maana yatakupa wingi wa siku, maisha marefu na fanaka kwa wingi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana yatakupa wingi wa siku, maisha marefu na fanaka kwa wingi. Neno: Bibilia Takatifu kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako na kukuletea mafanikio. Neno: Maandiko Matakatifu kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako na kukuletea mafanikio. BIBLIA KISWAHILI Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani. |
Nawe ukienda katika njia zangu, na kuyashika mausia yangu, na amri zangu, kama baba yako Daudi alivyokwenda, basi nitazifanya siku zako kuwa nyingi.
Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.
Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na muwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana vyenu nao, juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi.
Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na BWANA, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kulia wala wa kushoto.
Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.