Methali 21:21 - Swahili Revised Union Version Aandamaye haki na fadhili, Ataona uhai na haki na heshima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayepania uadilifu na huruma, ataishi maisha marefu na kuheshimiwa. Biblia Habari Njema - BHND Anayepania uadilifu na huruma, ataishi maisha marefu na kuheshimiwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayepania uadilifu na huruma, ataishi maisha marefu na kuheshimiwa. Neno: Bibilia Takatifu Yeye afuatiaye haki na upendo hupata uzima, mafanikio na heshima. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye afuatiaye haki na upendo hupata uzima, mafanikio na heshima. BIBLIA KISWAHILI Aandamaye haki na fadhili, Ataona uhai na haki na heshima. |
Nisikilizeni, ninyi mnaoifuatia haki; ninyi mnaomtafuta BWANA; uangalieni mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa, na tundu la shimo ambalo mlitolewa kwa kuchimbuliwa.
Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, subira, upole.
Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.