Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 15:9 - Swahili Revised Union Version

9 Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali humpenda mtu afuatiaye wema.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Mwenendo wa waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini Mungu huwapenda wale wafuatao mambo adili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Mwenendo wa waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini Mungu huwapenda wale wafuatao mambo adili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Mwenendo wa waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini Mungu huwapenda wale wafuatao mambo adili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Mwenyezi Mungu huchukia sana njia ya waovu, bali huwapenda wale wafuatao haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 bwana huchukia sana njia ya waovu, bali huwapenda wale wafuatao haki.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali humpenda mtu afuatiaye wema.

Tazama sura Nakili




Methali 15:9
21 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.


Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki, Apenda matendo ya haki, Wanyofu wa moyo watauona uso wake.


Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele.


Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako; Unawachukia wote watendao uovu.


Adhabu kali ina yeye aiachaye njia; Naye achukiaye kukemewa atakufa.


Aandamaye haki na fadhili, Ataona uhai na haki na heshima.


Mwenye kiburi na moyo wa majivuno, Taa yake ni dhambi.


Njia yake aliyelemewa na dhambi imepotoka sana; Bali mtu aliye safi, kazi yake ni sawasawa.


Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.


Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.


Njia yake mwenye haki ni unyofu; Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki.


Nisikilizeni, ninyi mnaoifuatia haki; ninyi mnaomtafuta BWANA; uangalieni mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa, na tundu la shimo ambalo mlitolewa kwa kuchimbuliwa.


Nisikilizeni, ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sheria yangu; msiogope masuto ya watu, wala msifadhaike kwa sababu ya dhihaka zao.


Tena nilituma kwenu watumishi wangu wote, manabii, nikiamka mapema na kuwatuma, nikisema, Basi ninyi; msilifanye chukizo hili linalochukiza.


Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.


Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;


Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.


naye atakupenda na kukubariki na kukuongeza tena ataubariki uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako, kuongezeka kwa ng'ombe na kondoo wako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwa atakupa.


Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, subira, upole.


Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo