Methali 21:2 - Swahili Revised Union Version Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huipima mioyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Matendo yote ya mtu ni sawa machoni pake, lakini Mwenyezi-Mungu hupima mioyo. Biblia Habari Njema - BHND Matendo yote ya mtu ni sawa machoni pake, lakini Mwenyezi-Mungu hupima mioyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Matendo yote ya mtu ni sawa machoni pake, lakini Mwenyezi-Mungu hupima mioyo. Neno: Bibilia Takatifu Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake, bali Mwenyezi Mungu huupima moyo. Neno: Maandiko Matakatifu Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake, bali bwana huupima moyo. BIBLIA KISWAHILI Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huipima mioyo. |
Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.
Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe; Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?
Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?
Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
Akawaambia, Ninyi ndinyi mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu awajua mioyo yenu; kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu.
nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye fikira na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.