Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira.
Methali 19:11 - Swahili Revised Union Version Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenye busara hakasiriki upesi; kusamehe makosa ni fahari kwake. Biblia Habari Njema - BHND Mwenye busara hakasiriki upesi; kusamehe makosa ni fahari kwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenye busara hakasiriki upesi; kusamehe makosa ni fahari kwake. Neno: Bibilia Takatifu Hekima ya mtu humpa uvumilivu, ni kwa utukufu wake kusamehe makosa. Neno: Maandiko Matakatifu Hekima ya mtu humpa uvumilivu, ni kwa utukufu wake kusamehe makosa. BIBLIA KISWAHILI Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa. |
Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira.
Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.
Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.
tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;