Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
Methali 18:2 - Swahili Revised Union Version Mpumbavu hapendezwi na ufahamu; Ila moyo wake udhihirike tu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mpumbavu hapendezwi na busara; kwake cha maana ni maoni yake tu. Biblia Habari Njema - BHND Mpumbavu hapendezwi na busara; kwake cha maana ni maoni yake tu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mpumbavu hapendezwi na busara; kwake cha maana ni maoni yake tu. Neno: Bibilia Takatifu Mpumbavu hafurahii ufahamu, bali hufurahia kutangaza maoni yake mwenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Mpumbavu hafurahii ufahamu, bali hufurahia kutangaza maoni yake mwenyewe. BIBLIA KISWAHILI Mpumbavu hapendezwi na ufahamu; Ila moyo wake udhihirike tu. |
Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?
Naam, huyo mpumbavu tena, aendapo njiani, hupungukiwa na fahamu zake; hata humwambia kila mtu ya kuwa yeye ni mpumbavu.
Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi aondoke katika nchi yao.
Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, jitahidini kusudi mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa.
Na kuhusu vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna ujuzi. Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga.
Wengine wanahubiri habari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina; na wengine kwa nia njema.