Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wakorintho 14:12 - Swahili Revised Union Version

12 Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, jitahidini kusudi mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Hali kadhalika na nyinyi, maadamu mna hamu ya kupata vipaji vya Roho, jitahidini hasa kujipatia vile vinavyosaidia kulijenga kanisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Hali kadhalika na nyinyi, maadamu mna hamu ya kupata vipaji vya Roho, jitahidini hasa kujipatia vile vinavyosaidia kulijenga kanisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Hali kadhalika na nyinyi, maadamu mna hamu ya kupata vipaji vya Roho, jitahidini hasa kujipatia vile vinavyosaidia kulijenga kanisa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Vivyo hivyo na ninyi. Kwa kuwa mnatamani kuwa na karama za rohoni, jitahidini kuzidi sana katika karama kwa ajili ya kuwajenga waumini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Vivyo hivyo na ninyi. Kwa kuwa mnatamani kuwa na karama za rohoni, jitahidini kuzidi sana katika karama kwa ajili ya kulijenga kundi la waumini.

Tazama sura Nakili




1 Wakorintho 14:12
9 Marejeleo ya Msalaba  

Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana.


Jitahidini sana kupata karama zilizo kuu. Na nitawaonesheni njia iliyo bora zaidi.


Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.


Ufuatilieni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kutoa unabii.


Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri.


Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.


Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kutoa unabii, maana yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.


ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo