Sulemani Akasema, Akionekana kuwa mtu wa kweli, hata unywele wake mmoja hautaanguka chini; lakini uovu ukionekana ndani yake, atakufa.
Methali 13:6 - Swahili Revised Union Version Haki humlinda yeye aliye mnyofu katika njia yake; Bali ubaya humwangusha mwenye dhambi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uadilifu huwalinda wenye mwenendo mnyofu, lakini dhambi huwaangusha waovu. Biblia Habari Njema - BHND Uadilifu huwalinda wenye mwenendo mnyofu, lakini dhambi huwaangusha waovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uadilifu huwalinda wenye mwenendo mnyofu, lakini dhambi huwaangusha waovu. Neno: Bibilia Takatifu Haki humlinda mtu mwadilifu, bali uovu humwangusha mwenye dhambi. Neno: Maandiko Matakatifu Haki humlinda mtu mwadilifu, bali uovu humwangusha mwenye dhambi. BIBLIA KISWAHILI Haki humlinda yeye aliye mnyofu katika njia yake; Bali ubaya humwangusha mwenye dhambi. |
Sulemani Akasema, Akionekana kuwa mtu wa kweli, hata unywele wake mmoja hautaanguka chini; lakini uovu ukionekana ndani yake, atakufa.
Kila aliyetaka akamweka wakfu, ili wawepo makuhani wa mahali pa juu. Jambo hilo likawa dhambi kwa nyumba ya Yeroboamu, hata kuiharibu, na kuifuta usoni pa nchi.
Maana aliitolea dhabihu miungu ya Dameski iliyompiga, akasema, Kwa sababu miungu ya wafalme wa Shamu imewasaidia wao, mimi nitaitolea dhabihu, ili inisaidie mimi. Lakini ndiyo iliyomwangamiza yeye na Israeli wote.
Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.