Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 11:20 - Swahili Revised Union Version

20 Wenye uhalifu moyoni ni chukizo kwa BWANA; Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Wenye nia mbaya ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini wenye mwenendo mwema ni furaha yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Wenye nia mbaya ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini wenye mwenendo mwema ni furaha yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Wenye nia mbaya ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini wenye mwenendo mwema ni furaha yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Mwenyezi Mungu huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu, bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 bwana huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu, bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

20 Wenye uhalifu moyoni ni chukizo kwa BWANA; Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza.

Tazama sura Nakili




Methali 11:20
20 Marejeleo ya Msalaba  

Nami ninajua, Mungu wangu, ya kuwa wewe wajaribu moyo, nawe wapendezwa na unyofu. Nami katika unyofu wa moyo wangu nimeyatoa haya yote kwa hiari yangu mwenyewe; nami sasa nimeona kwa furaha watu wako, waliopo hapa, wakikutolea kwa hiari yao.


Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu, Lililo ovu sitalijua.


Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki, Apenda matendo ya haki, Wanyofu wa moyo watauona uso wake.


Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya BWANA.


Hakika wenye haki watalishukuru jina lako, Wenye adili watakaa mahali ulipo Wewe.


Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanifundisha hekima kwa siri,


Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu; Bali wazawa wa wenye haki wataokoka.


Midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake.


Haki humlinda yeye aliye mnyofu katika njia yake; Bali ubaya humwangusha mwenye dhambi.


Wapumbavu huidharau hatia; Bali upo upendeleo kwa wenye haki.


Ushauri mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali maneno yapendezayo ni safi.


Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.


Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.


Asiye haki huufanya uso wake kuwa mgumu; Bali mtu mnyofu huzifikiri njia zake.


Maana mtu mjeuri ni chukizo kwa BWANA, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.


Mna upotovu moyoni mwake, hutunga uovu daima, Hupanda mbegu za magomvi.


Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.


Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha; Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo