Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Ndivyo alivyo mwanamke mzuri asiye na akili.
Methali 12:4 - Swahili Revised Union Version Mwanamke mwema ni taji la mumewe; Bali aaibishaye ni kama kuoza mifupani mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mke mwema ni taji ya fahari kwa mumewe; amwaibishaye mumewe ni kama kidonda mifupani mwake. Biblia Habari Njema - BHND Mke mwema ni taji ya fahari kwa mumewe; amwaibishaye mumewe ni kama kidonda mifupani mwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mke mwema ni taji ya fahari kwa mumewe; amwaibishaye mumewe ni kama kidonda mifupani mwake. Neno: Bibilia Takatifu Mke mwenye tabia nzuri ni taji la mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa ya mumewe. Neno: Maandiko Matakatifu Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa ya mumewe. BIBLIA KISWAHILI Mwanamke mwema ni taji la mumewe; Bali aaibishaye ni kama kuoza mifupani mwake. |
Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Ndivyo alivyo mwanamke mzuri asiye na akili.
Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.
Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.
Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.
Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana watu wote wa mjini wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema.