Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 12:4 - BIBLIA KISWAHILI

4 Mwanamke mwema ni taji la mumewe; Bali aaibishaye ni kama kuoza mifupani mwake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Mke mwema ni taji ya fahari kwa mumewe; amwaibishaye mumewe ni kama kidonda mifupani mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Mke mwema ni taji ya fahari kwa mumewe; amwaibishaye mumewe ni kama kidonda mifupani mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Mke mwema ni taji ya fahari kwa mumewe; amwaibishaye mumewe ni kama kidonda mifupani mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Mke mwenye tabia nzuri ni taji la mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa ya mumewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa ya mumewe.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

4 Mke mwema ni taji ya fahari kwa mumewe; amwaibishaye mumewe ni kama kidonda mifupani mwake.

Tazama sura Nakili




Methali 12:4
16 Marejeleo ya Msalaba  

Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Ndivyo alivyo mwanamke mzuri asiye na akili.


Mawazo ya mwenye haki ni adili; Bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa.


Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.


Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa.


Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA.


Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.


Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.


Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo; Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake.


Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.


Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.


Lakini, katika Bwana si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke.


Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.


Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana watu wote wa mjini wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo