Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu.
Methali 12:24 - Swahili Revised Union Version Mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipishwa kodi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kuwa na bidii kutampa mtu cheo, lakini uvivu utamfanya mtumwa. Biblia Habari Njema - BHND Kuwa na bidii kutampa mtu cheo, lakini uvivu utamfanya mtumwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kuwa na bidii kutampa mtu cheo, lakini uvivu utamfanya mtumwa. Neno: Bibilia Takatifu Mikono yenye bidii itatawala, bali uvivu huishia katika kazi za utumwa. Neno: Maandiko Matakatifu Mikono yenye bidii itatawala, bali uvivu huishia katika kazi za utumwa. BIBLIA KISWAHILI Mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipishwa kodi. |
Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu.
Na huyo Yeroboamu alikuwa mtu hodari, shujaa; Sulemani akaona ya kuwa kijana huyo ni mtu mwenye bidii, akamweka juu ya kazi yote ya nyumba ya Yusufu.
Ikawa, Israeli wote waliposikia ya kwamba Yeroboamu amerudi, wakapeleka watu wakamwita aje mkutanoni, wakamfanya mfalme juu ya Israeli wote; wala hapakuwa na mtu aliyeshikamana na nyumba ya Daudi, ila kabila la Yuda peke yake.
watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuweza kuwaharibu kabisa, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo.
Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu; Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu.
Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.
Kisha ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamepata nguvu, ndipo walipowatia hao Wakanaani katika kazi ya shokoa, wala hawakuwafukuza kabisa.