Methali 10:19 - Swahili Revised Union Version Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Penye maneno mengi hapakosekani makosa, lakini aneyeuzuia ulimi wake ana busara. Biblia Habari Njema - BHND Penye maneno mengi hapakosekani makosa, lakini aneyeuzuia ulimi wake ana busara. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Penye maneno mengi hapakosekani makosa, lakini aneyeuzuia ulimi wake ana busara. Neno: Bibilia Takatifu Dhambi haiondolewi kwa maneno mengi, bali wenye busara huzuia ulimi wao. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani, lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara. BIBLIA KISWAHILI Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili. |
Nilisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya awapo mbele yangu.
Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya.
Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu; kwa maana, Mungu yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache.
Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.
Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.