Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 39:1 - Swahili Revised Union Version

1 Nilisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya awapo mbele yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Nilisema: “Nitayachunga maisha yangu, nisije nikatenda dhambi kwa usemi wangu. Nitafunga mdomo wangu waovu wawapo karibu nami.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Nilisema: “Nitayachunga maisha yangu, nisije nikatenda dhambi kwa usemi wangu. Nitafunga mdomo wangu waovu wawapo karibu nami.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Nilisema: “Nitayachunga maisha yangu, nisije nikatenda dhambi kwa usemi wangu. Nitafunga mdomo wangu waovu wawapo karibu nami.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi; nitaweka lijamu kinywani mwangu wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi; nitaweka lijamu kinywani mwangu wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.”

Tazama sura Nakili




Zaburi 39:1
21 Marejeleo ya Msalaba  

ili BWANA afanye imara neno lake alilonena kuhusu habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli.


Lakini Yehu hakuangalia, aende katika sheria ya BWANA, Mungu wa Israeli, kwa moyo wake wote; hakutoka katika makosa ya Yeroboamu, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli.


na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru BWANA, kwa kuwa fadhili zake ni za milele;


Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.


Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.


Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu?


Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.


Uuzuie ulimi wako na mabaya, Na midomo yako na kusema hila.


Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa utulivu, Wokovu wangu hutoka kwake.


Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia.


Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.


Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu.


Kwa ajili ya hayo mwenye busara atanyamaza kimya wakati kama huo; kwa kuwa ni wakati mbaya.


Nendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.


Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo tuliyoyasikia tusije tukayakosa.


Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, ili hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo