Marko 4:23 - Swahili Revised Union Version Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenye masikio na asikie!” Biblia Habari Njema - BHND Mwenye masikio na asikie!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenye masikio na asikie!” Neno: Bibilia Takatifu Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.” Neno: Maandiko Matakatifu Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.” BIBLIA KISWAHILI Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie. |
Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie.
Nyingine zikaanguka penye udongo mzuri; zikamea, zikazaa moja kwa mia. Alipokuwa akinena hayo alipaza sauti akisema, Mwenye masikio ya kusikizia, na asikie.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.