Lakini Abishai, mwana wa Seruya, akamsaidia, akampiga Mfilisti, akamwua. Ndipo watu wa Daudi wakamwapia, wakasema, Wewe hutatoka tena pamoja nasi kwenda vitani, usije ukaizima taa ya Israeli.
2 Samueli 22:29 - Swahili Revised Union Version Kwa kuwa wewe u taa yangu, Ee BWANA; Na BWANA ataniangazia giza langu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Mwenyezi-Mungu, wewe u taa yangu, Mungu wangu, unayefukuza giza langu. Biblia Habari Njema - BHND Ee Mwenyezi-Mungu, wewe u taa yangu, Mungu wangu, unayefukuza giza langu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Mwenyezi-Mungu, wewe u taa yangu, Mungu wangu, unayefukuza giza langu. Neno: Bibilia Takatifu Wewe ni taa yangu, Ee Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hulifanya giza langu kuwa mwanga. Neno: Maandiko Matakatifu Wewe ni taa yangu, Ee bwana. bwana hulifanya giza langu kuwa mwanga. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa wewe u taa yangu, Ee BWANA; Na BWANA ataniangazia giza langu. |
Lakini Abishai, mwana wa Seruya, akamsaidia, akampiga Mfilisti, akamwua. Ndipo watu wa Daudi wakamwapia, wakasema, Wewe hutatoka tena pamoja nasi kwenda vitani, usije ukaizima taa ya Israeli.
Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko.
Hapo taa yake ilipomulika juu yangu kichwani, Nami nilitembea gizani kwa njia ya mwanga wake;
BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?
Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
Ni nani miongoni mwenu amchaye BWANA, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la BWANA, na kumtegemea Mungu wake.
Nitaivumilia ghadhabu ya BWANA, kwa kuwa nimemwasi; hata atakaponitetea shutuma yangu, na kunifanyia hukumu; atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki yake.
Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawachomozea, likiwa na uwezo wa kuponya katika miale yake; nanyi mtatoka nje, na kuchezacheza kama ndama watokapo mazizini.
Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-kondoo.