Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mika 7:9 - Swahili Revised Union Version

9 Nitaivumilia ghadhabu ya BWANA, kwa kuwa nimemwasi; hata atakaponitetea shutuma yangu, na kunifanyia hukumu; atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Kwa vile nimemkosea Mwenyezi-Mungu, sina budi kuvumilia ghadhabu yake, mpaka atakapotetea kisa changu na kunijalia haki yangu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaona akithibitisha haki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Kwa vile nimemkosea Mwenyezi-Mungu, sina budi kuvumilia ghadhabu yake, mpaka atakapotetea kisa changu na kunijalia haki yangu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaona akithibitisha haki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Kwa vile nimemkosea Mwenyezi-Mungu, sina budi kuvumilia ghadhabu yake, mpaka atakapotetea kisa changu na kunijalia haki yangu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaona akithibitisha haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake, nitabeba ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, hadi atakapotetea shauri langu na kuithibitisha haki yangu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaiona haki yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake, nitabeba ghadhabu ya bwana, mpaka atakaponitetea shauri langu na kuithibitisha haki yangu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaiona haki yake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Nitaivumilia ghadhabu ya BWANA, kwa kuwa nimemwasi; hata atakaponitetea shutuma yangu, na kunifanyia hukumu; atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki yake.

Tazama sura Nakili




Mika 7:9
36 Marejeleo ya Msalaba  

Daudi, alipomwona malaika aliyewapiga watu, akanena na BWANA, akasema, Tazama, ni mimi niliyekosa, ni mimi niliyepotoka; lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Mkono wako na uwe juu yangu, na juu ya nyumba ya baba yangu.


Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.


Sembuse usemapo wewe ya kuwa humwangalii, Hiyo kesi i mbele yake, nawe wamngojea!


Unitetee na kunikomboa, Unihuishe sawasawa na ahadi yako.


Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama jina la adhuhuri.


Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki, Uniokoe kutoka kwa mtu wa hila asiye haki.


BWANA uondoke kwa hasira yako; Ujiinue Juu ya ujeuri wa watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu.


Maana hukumu itarejea kwa wenye haki, Na wote walio wanyofu wa moyo wataifuata.


Nitawaleta vipofu kwa njia wasiyoijua; katika mapito wasiyoyajua nitawaongoza; nitafanya giza kuwa nuru mbele yao; na mahali palipopotoka kuwa pamenyoka. Haya nitayatenda, wala sitawaacha.


kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.


Mimi ninaleta karibu haki yangu, haitakuwa mbali, na wokovu wangu hautakawia; nami nitaweka wokovu katika Sayuni kwa ajili ya Israeli, utukufu wangu.


BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevyalevya, hilo bakuli la hasira yangu; hutalinywea tena;


BWANA asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu uko karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa.


Ole wangu, kwa sababu ya jeraha langu! Pigo langu laumia; lakini nilisema, Kweli, ni huzuni yangu mimi, nami sina budi kuivumilia.


Ijapokuwa maovu yetu yanatushuhudia, lakini utende wewe kwa ajili ya jina lako, Ee BWANA, maana kurudi nyuma kwetu ni kwingi; tumekutenda dhambi.


BWANA ameitokeza haki yetu; Njooni, tutangaze katika Sayuni Habari za kazi ya BWANA, Mungu wetu.


BWANA ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka.


mimi nami nimewaendea kinyume, na kuwatia katika nchi ya adui zao; lakini hapo, kama mioyo yao isiyokuwa tohara ikinyenyekea, nao wakubali adhabu ya uovu wao;


Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.


Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


baada ya hayo nimewekewa taji la haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.


Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.


Basi BWANA atuamue, akatuhukumu mimi na wewe, akaone, akanitetee neno langu, akaniokoe kutokana na mkono wako.


Naye Daudi aliposikia ya kwamba Nabali amekufa, alisema, Na ahimidiwe BWANA ambaye amenitetea teto la shutumu langu mkononi mwa Nabali, na kumzuia mtumishi wake asitende maovu; tena uovu wake Nabali BWANA amemrudishia juu ya kichwa chake mwenyewe. Kisha Daudi akatuma watu, akamposa Abigaili ili amwoe.


Daudi akasema, Aishivyo BWANA, BWANA atampiga; au siku yake ya kufa itampata; atashuka kwenda vitani na kupotea.


Basi Samweli akamwambia kila neno, asimfiche lolote. Naye akasema, Ndiye BWANA; na afanye alionalo kuwa ni jema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo