Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Nehemia 7 - Swahili Revised Union Version

1 Ikawa, baada ya ukuta kujengwa, na milango kuisimamishwa na kuweka mabawabu, waimbaji na Walawi,

2 ndipo nilimteua ndugu yangu Hanani, kuwa mwangalizi wa Yerusalemu akisaidiana na Hanania, jemadari wa ngome, kwa maana alikuwa mtu mwaminifu na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi.

3 Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla jua halijachomoza; na kabla walinzi hawajaondoka waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake.

4 Basi mji ulikuwa wa nafasi nyingi, tena mkubwa; lakini watu waliomo walikuwa wachache, na nyumba zilikuwa hazijajengwa.


Orodha ya waliotoka uhamishoni

5 Mungu wangu akanitia moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na maofisa, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba. Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo;

6 Hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake;

7 ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo idadi ya watu wa watu wa Israeli;

8 Wana wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili.

9 Wana wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili.

10 Wana wa Ara mia sita hamsini na wawili.

11 Wana wa Pahath-Moabu, wa wana wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wanane.

12 Wana wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.

13 Wana wa Zatu, mia nane arubaini na watano.

14 Wana wa Zakai, mia saba na sitini.

15 Wana wa Binui, mia sita arubaini na wanane.

16 Wana wa Bebai, mia sita ishirini na wanane.

17 Wana wa Azgadi, elfu mbili mia tatu ishirini na wawili.

18 Wana wa Adonikamu, mia sita sitini na saba.

19 Wana wa Bigwai, elfu mbili sitini na saba.

20 Wana wa Adini, mia sita hamsini na watano.

21 Wana wa Ateri, wa Hezekia, tisini na wanane.

22 Wana wa Hashumu, mia tatu ishirini na wanane.

23 Wana wa Besai, mia tatu ishirini na wanne.

24 Wana wa Harifu, mia moja na kumi na wawili.

25 Wana wa Gibeoni, tisini na watano.

26 Watu wa Bethlehemu na Netofa, mia moja na themanini na wanane.

27 Watu wa Anathothi, mia moja ishirini na wanane.

28 Watu wa Beth-Azmawethi, arubaini na wawili.

29 Watu wa Kiriath-Yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arubaini na watatu.

30 Watu wa Rama na Geba, mia sita na ishirini na mmoja.

31 Watu wa Mikmashi, mia moja na ishirini na wawili.

32 Watu wa Betheli na Ai, mia moja ishirini na watatu.

33 Watu wa Nebo, hamsini na wawili.

34 Wana wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.

35 Wana wa Harimu, mia tatu na ishirini.

36 Wana wa Yeriko, mia tatu arubaini na watano.

37 Wana wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na mmoja.

38 Watu wa Senaa, elfu tatu mia tisa na thelathini.

39 Makuhani; Wana wa Yedaya, wa mbari ya Yeshua, mia tisa sabini na watatu.

40 Wana wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili.

41 Wana wa Pashuri, elfu moja mia mbili arubaini na saba.

42 Wana wa Harimu, elfu moja na kumi na saba.

43 Walawi; Wana wa Yeshua, wa Kadmieli wa wana wa Hodavia, sabini na wanne.

44 Waimbaji; Wana wa Asafu, mia moja arubaini na wanane.

45 Mabawabu; Wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai, mia moja thelathini na wanane.

46 Wanethini; wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi;

47 wana wa Kerosi, wana wa Siaha, wana wa Padoni;

48 wana wa Lebana, wana wa Hagaba, wana wa Salmai;

49 wana wa Hanani, wana wa Gideli, wana wa Gahari;

50 wana wa Reaya, wana wa Resini, wana wa Nekoda;

51 wana wa Gazamu, wana wa Uza, wana wa Pasea;

52 wana wa Besai wana wa Meunimu, wana wa Nefusimu;

53 wana wa Bakbuki, wana wa Hakufa, wana wa Harhuri;

54 wana wa Basluthi, wana wa Mehida, wana wa Harsha;

55 wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema;

56 wana wa Nesia, wana wa Hatifa.

57 Wazawa wa watumishi wa Sulemani; Wana wa Sotai, wana wa Soferethi, wana wa Peruda;

58 wana wa Yaala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli;

59 wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereth-Sebaimu, wana wa Amoni.

60 Wanethini wote, pamoja na wazawa wa watumishi wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili.

61 Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; lakini hawakuweza kuonesha mbari za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli;

62 Wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda, mia sita na arubaini na wawili.

63 Tena katika makuhani; Wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti za Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao.

64 Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi.

65 Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vile vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu.

66 Basi hilo kusanyiko lote zima, jumla yake ilikuwa watu elfu arubaini na mbili, mia tatu na sitini,

67 tena zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wanaume kwa wanawake, ambao walikuwa elfu saba na mia tatu na thelathini na saba; kisha walikuwa na waimbaji wanaume kwa wanawake mia mbili arubaini na watano.

68 Farasi wao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu zao, mia mbili arubaini na watano;

69 ngamia wao, mia nne thelathini na watano; punda zao, elfu sita na mia saba na ishirini.

70 Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa walitoa mali kwa ajili ya kazi hii. Yule Tirshatha akatoa kwa ajili ya hazina darkoni, za dhahabu elfu moja, na mabeseni hamsini, na mavazi ya makuhani mia tano na thelathini.

71 Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa wakatoa, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu elfu ishirini, na mane za fedha elfu mbili na mia mbili.

72 Na mabaki ya watu wakatoa darkoni za dhahabu elfu ishirini, na mane za fedha elfu mbili, na mavazi ya makuhani sitini na saba.

73 Hivyo makuhani, na Walawi, na mabawabu, na waimbaji, na baadhi ya watu, na Wanethini, na Israeli wote, wakakaa mijini mwao. Hata ulipowadia mwezi wa saba, wana wa Israeli walikuwa wakikaa katika miji yao.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Bible Society of Kenya
Tufuate:



Matangazo