Mistari ya Biblia

Matangazo


Vikundi Vidogo

MISTARI KUHUSU TUMAINI

Tumaini ni muhimu sana maishani mwetu. Weka tumaini lako kwa Mungu, amini utaona matamanio ya moyo wako yakitimia. Dumisha ari hiyo, mzuka huo wa kusonga mbele hadi utimize ulilokusudia. Usikate tamaa, na uyaweke yote unayoyatamani mikononi mwa Baba yetu wa Mbinguni.

Kama Mkristo, usisahau kamwe tumaini la kumuona Bwana wetu uso kwa uso, na kwamba kwa sababu ya sadaka aliyotoa Bwana Yesu Kristo, umeokolewa kwa neema, na tutakuwa naye milele. Tumaini kwa Mungu linakuondolea hofu ya yajayo na mashaka, mwamini Mungu siku zote, atakupatia nguvu za


Wimbo Ulio Bora 8:6-7

Nipige kama mhuri moyoni mwako, naam, kama mhuri mikononi mwako. Maana pendo lina nguvu kama kifo, wivu nao ni mkatili kama kaburi. Mlipuko wake ni kama mlipuko wa moto, huwaka kama mwali wa moto.

Maji mengi hayawezi kamwe kulizima, mafuriko hayawezi kulizamisha. Mtu akijaribu kununua pendo, akalitolea mali yake yote, atakachopata ni dharau tupu.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 1:16

Hakika u mzuri ewe nikupendaye, u mzuri kweli! Majani mabichi yatakuwa kitanda chetu;

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 4:7

Tazama ulivyo mzuri ee mpenzi wangu, wewe huna kasoro yoyote.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 4:9

Umefurahisha moyo wangu, dada yangu, bi arusi, umefurahisha moyo wangu, kwa kunitupia jicho mara moja tu, na kwa huo mkufu wako shingoni.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 4:10

Dada yangu, bi arusi; pendo lako ni tamu ajabu. Ni bora kuliko divai, marashi yako yanukia kuliko viungo vyote.

Sura   |  Matoleo
1 Wakorintho 13:8

Upendo hauna kikomo kamwe. Kama kuna vipaji vya kutangaza ujumbe wa Mungu, hivyo vitatoweka siku moja; kama ni vipaji vya kusema lugha ngeni, vitakoma; kama kuna elimu, nayo itapita.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 1:4

Nichukue, twende zetu haraka, mfalme amenileta katika chumba chake. Tutafurahi na kushangilia kwa sababu yako, tutasifu mapenzi yako kuliko divai. Wanawake wana haki kukupenda!

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 1:15

Hakika u mzuri, ee mpenzi wangu, hakika u mzuri! Macho yako ni kama ya hua!

Sura   |  Matoleo
Methali 18:22

Anayempata mke amepata bahati njema; hiyo ni fadhili kutoka kwa Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo
Mhubiri 4:12

Mtu akiwa peke yake aweza kushindwa na adui, lakini wakiwa wawili watamkabili na kumshinda adui. Kamba tatu zikisokotwa pamoja hazikatiki kwa urahisi.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 1:2

Heri midomo yako inibusu, maana pendo lako ni bora kuliko divai.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 8:7

Maji mengi hayawezi kamwe kulizima, mafuriko hayawezi kulizamisha. Mtu akijaribu kununua pendo, akalitolea mali yake yote, atakachopata ni dharau tupu.

Sura   |  Matoleo
1 Wakorintho 13:4-7

Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni.

Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya,

hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli.

Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote.

Sura   |  Matoleo
Wakolosai 3:14

Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo, kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 2:16

Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake. Yeye hulisha kondoo wake penye yungiyungi,

Sura   |  Matoleo
1 Wakorintho 13:13

Sasa yanadumu haya matatu: Imani, tumaini na upendo; lakini lililo kuu kupita yote ni upendo.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 8:6

Nipige kama mhuri moyoni mwako, naam, kama mhuri mikononi mwako. Maana pendo lina nguvu kama kifo, wivu nao ni mkatili kama kaburi. Mlipuko wake ni kama mlipuko wa moto, huwaka kama mwali wa moto.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 6:3

Mimi ni wake mpenzi wangu, naye ni wangu; yeye huwalisha kondoo wake penye yungiyungi.

Sura   |  Matoleo
Mwanzo 2:24

Ndiyo maana mwanamume humwacha baba yake na mama yake, akaambatana na mkewe, nao wawili huwa mwili mmoja.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 2:5

Nishibishe na zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, maana naugua kwa mapenzi!

Sura   |  Matoleo
Wakolosai 3:19

Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao.

Sura   |  Matoleo
Waefeso 5:33

Lakini yanawahusu nyinyi pia: Kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.

Sura   |  Matoleo
Methali 10:12

Chuki huzusha ugomvi, lakini upendo hufunika makosa yote.

Sura   |  Matoleo
Methali 31:11-12

Mumewe humwamini kwa moyo, kwake atapata faida daima.

Kamwe hamtendei mumewe mabaya, bali humtendea mema maisha yake yote.

Sura   |  Matoleo
1 Yohana 4:19

Sisi tuna upendo kwa sababu Mungu alitupenda kwanza.

Sura   |  Matoleo
1 Wathesalonike 3:12

Bwana awawezeshe nyinyi kupendana na kuwapenda watu wote zaidi na zaidi, kama vile sisi tunavyowapenda nyinyi.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 2:2

Kama yungiyungi kati ya michongoma, ndivyo alivyo mpenzi wangu kati ya wasichana.

Sura   |  Matoleo
1 Yohana 4:17

Upendo umekamilika ndani yetu kusudi tuweze kuwa na ujasiri siku ile ya hukumu; kwani maisha yetu hapa duniani ni kama yale ya Kristo.

Sura   |  Matoleo
1 Petro 4:8

Zaidi ya yote pendaneni kwa moyo wote, maana upendo hufunika dhambi nyingi.

Sura   |  Matoleo
1 Yohana 4:18

Palipo na upendo hapana woga; naam, upendo kamili hufukuza woga wote. Basi, mtu mwenye woga hajakamilika bado katika upendo, kwani woga huhusikana na adhabu.

Sura   |  Matoleo
Mwanzo 2:18

Kisha Mwenyezi-Mungu akasema, “Si vizuri huyu mwanamume kuwa peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.”

Sura   |  Matoleo
Waefeso 5:25-28

Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake.

Alifanya hivyo ili kwa neno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baada ya kulifanya safi kwa kuliosha katika maji,

kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safi kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo.

Basi, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. (

Sura   |  Matoleo
Yohana 15:12

Hii ndiyo amri yangu: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 2:3

Kama mtofaa kati ya miti ya msituni, ndivyo alivyo mpenzi wangu kati ya wavulana. Nafurahia kuketi chini ya kivuli chake, na tunda lake tamu sana kwangu.

Sura   |  Matoleo
Mwanzo 29:20

Basi, Yakobo akamtumikia Labani miaka saba kwa ajili ya Raheli, lakini kwake muda huo ulikuwa kama siku chache, kwa vile alivyompenda Raheli.

Sura   |  Matoleo
Methali 3:3-4

Utii na uaminifu visitengane nawe. Vifunge shingoni mwako; viandike moyoni mwako.

Usigombane na mtu bila sababu ikiwa hajakudhuru kwa lolote.

Usimwonee wivu mtu mkatili, wala usiige mwenendo wake.

Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu.

Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu, lakini huyabariki makao ya waadilifu.

Yeye huwadharau wenye dharau, lakini huwafadhili wanyenyekevu.

Wenye hekima watavuna heshima, lakini wapumbavu watapata fedheha.

Hivyo utakubalika na kusifika, mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu.

Sura   |  Matoleo
Waefeso 5:25

Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 3:4

Mara tu nilipoachana nao, nilimwona mpenzi wangu wa moyo; nikamshika wala sikumwachia aondoke, hadi nilipompeleka nyumbani kwa mama yangu, hadi chumbani kwake yule aliyenizaa.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 37:4

Uitafute furaha yako kwa Mwenyezi-Mungu, naye atakujalia unayotamani moyoni.

Sura   |  Matoleo
Methali 5:18

Chemchemi yako na ibarikiwe, umfurahie mke uliyemwoa ukiwa kijana.

Sura   |  Matoleo
Mhubiri 9:9

Furahia maisha pamoja na mke wako umpendaye muda wote wa maisha yako ya bure ambayo Mungu amekujalia hapa duniani; maana hilo ndilo ulilopangiwa maishani, katika kazi zako hapa duniani.

Sura   |  Matoleo
Wafilipi 1:3-5

Namshukuru Mungu wangu kila ninapowakumbukeni;

Sasa mwaweza kushirikiana nami katika kupigana vita. Vita hivi ni vile mlivyoona nikipigana pale awali na ambavyo bado napigana sasa kama mnavyosikia.

na kila ninapowaombeeni nyote, nasali kwa furaha,

kwa sababu ya jinsi mlivyonisaidia katika kazi ya Injili tangu siku ile ya kwanza mpaka leo.

Sura   |  Matoleo
Mathayo 19:4-6

Yesu akawajibu, “Je, hamkusoma katika Maandiko Matakatifu kwamba Mungu aliyemuumba mtu tangu mwanzo alimfanya mwanamume na mwanamke,

na akasema: ‘Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja?’

Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja. Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asikitenganishe.”

Sura   |  Matoleo
Methali 17:17

Rafiki wa kweli ni rafiki siku zote, ndugu huzaliwa asaidie wakati wa taabu.

Sura   |  Matoleo
Wagalatia 5:13-14

Nyinyi ndugu, mliitwa muwe watu huru. Lakini uhuru huo usiwe kisingizio cha kutawaliwa na tamaa za kidunia; ila mnapaswa kutumikiana kwa upendo.

Maana sheria yote hutimizwa katika kushika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”

Sura   |  Matoleo
Waroma 13:10

Ampendaye jirani yake hamtendei vibaya. Basi, upendo ni utimilifu wa sheria.

Sura   |  Matoleo
1 Yohana 3:18

Watoto wangu, upendo wetu usiwe maneno matupu, bali uwe upendo wa kweli na wa vitendo.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 85:10

Fadhili zake na uaminifu vitakutana; uadilifu na amani vitaungana.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 7:10

Mimi ni wake mpenzi wangu, naye anionea sana shauku.

Sura   |  Matoleo
Methali 31:10

Mke mwema kweli, apatikana wapi? Huyo ana thamani kuliko johari!

Sura   |  Matoleo
Waefeso 4:2-3

Muwe daima wanyenyekevu, wapole na wenye saburi; vumilianeni nyinyi kwa nyinyi kwa mapendo.

Lakini nyinyi hamkujifunza hivyo juu ya Kristo.

Ni dhahiri kwamba mlisikia barabara habari zake, na mkiwa wafuasi wake mkafundishwa ukweli ulivyo katika Yesu.

Basi, acheni mwenendo wenu wa awali, yaani ule utu wenu wa kale uliokuwa unaangamizwa kwa tamaa zake danganyifu.

Jirekebisheni upya rohoni na katika fikira zenu.

Vaeni hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayo hujionesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu.

Kwa hiyo, acheni uongo. Kila mmoja anapaswa kumwambia mwenzake ukweli, maana kila mmoja wetu ni kiungo cha mwili wa Kristo.

Kama mkikasirika, msikubali hasira yenu iwafanye mtende dhambi, na wala msikae na hasira kutwa nzima.

Msimpe Ibilisi nafasi.

Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini.

Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu.

Fanyeni bidii ya kuhifadhi umoja uletwao na Roho kwa kuzingatia amani iliyo kati yenu.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 5:16

Kinywa chake kimejaa maneno matamu, kwa ujumla anapendeza. Basi, hivyo ndivyo alivyo mpenzi wangu, naam, ndivyo alivyo rafiki yangu, enyi wanawake wa Yerusalemu.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 119:32

Nitafuata maelekezo ya amri zako, maana unanipa maarifa zaidi.

Sura   |  Matoleo
Waroma 15:5-6

Mungu aliye msingi wa saburi na faraja yote, awajalieni nyinyi kuwa na msimamo mmoja kufuatana na mfano wake Kristo Yesu,

ili nyinyi nyote, kwa nia moja na sauti moja, mumtukuze Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Sura   |  Matoleo
Wagalatia 5:22-23

Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu,

upole na kiasi. Hakuna sheria inayoweza kupinga mambo hayo.

Sura   |  Matoleo
1 Wakorintho 16:14

Kila mfanyacho kifanyike kwa upendo.

Sura   |  Matoleo
Zaburi 143:8

Asubuhi unioneshe fadhili zako, maana nimekuwekea tumaini langu. Unifundishe mwenendo wa kufuata, maana nakuelekezea ombi la moyo wangu.

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 1:2-3

Heri midomo yako inibusu, maana pendo lako ni bora kuliko divai.

Manukato yako yanukia vizuri, na jina lako ni kama marashi yaliyomiminwa. Kwa hiyo wanawake hukupenda!

Sura   |  Matoleo
Mathayo 22:39

Ya pili inafanana na hiyo: ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe’.

Sura   |  Matoleo
Methali 31:10-12

Mke mwema kweli, apatikana wapi? Huyo ana thamani kuliko johari!

Mumewe humwamini kwa moyo, kwake atapata faida daima.

Kamwe hamtendei mumewe mabaya, bali humtendea mema maisha yake yote.

Sura   |  Matoleo
1 Timotheo 5:1-2

Usimkemee mwanamume mzee, bali msihi kama vile angekuwa baba yako. Watendee vijana wa kiume kama ndugu zako,

na awe mwenye sifa nzuri: Aliyewalea watoto wake vizuri, aliyewakaribisha wageni nyumbani kwake, aliyewaosha miguu watu wa Mungu, aliyewasaidia watu wenye taabu, na aliyejitolea kufanya mambo mema.

Usiwaandikishe wajane vijana, kwani kama tamaa zao za maumbile zikizidi kuwa na nguvu zaidi kuliko kujitolea kwao kwa Kristo, watataka kuolewa tena,

na wataonekana kukosa uaminifu kuhusu ahadi yao ya pale awali.

Wajane kama hao huanza kupoteza wakati wao wakizurura nyumba hata nyumba; tena ubaya zaidi ni kwamba huanza kuwasengenya watu, na kujitia katika mambo ya watu wengine, huku wakisema mambo ambayo hawangepaswa kusema.

Kwa hiyo ningependelea wajane vijana waolewe, wapate watoto na kutunza nyumba zao ili maadui zetu wasipewe nafasi ya kusema mambo maovu juu yetu.

Kwa maana wajane wengine wamekwisha potoka na kumfuata Shetani.

Lakini kama mama Mkristo anao wajane katika jamaa yake, yeye anapaswa kuwatunza na si kuliachia kanisa mzigo huo, ili kanisa liweze kuwatunza wajane wale waliobaki peke yao kabisa.

Viongozi wa kanisa wanaowaongoza watu vizuri wanastahili kupata riziki maradufu, hasa wale wanaofanya bidii katika kuhubiri na kufundisha.

Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Usimfunge ng'ombe kinywa anapopura nafaka,” na tena “Mfanyakazi astahili malipo yake.”

Usikubali kupokea mashtaka dhidi ya mzee yasipowakilishwa na mashahidi wawili au watatu.

wanawake wazee kama mama zako, na vijana wa kike kama dada zako, kwa usafi wote.

Sura   |  Matoleo
1 Petro 3:7

Kadhalika nanyi waume, katika kuishi na wake zenu mnapaswa kutambua kwamba wao ni dhaifu na hivyo muwatendee kwa heshima; maana nao pia watapokea pamoja nanyi zawadi ya uhai anaowapeni Mungu. Hapo sala zenu hazitatiliwa kizuizi.

Sura   |  Matoleo
Waroma 12:10

Pendaneni kindugu; kila mmoja amfikirie kwanza mwenzake kwa heshima.

Sura   |  Matoleo
1 Yohana 4:7

Wapenzi wangu, tupendane, maana upendo hutoka kwa Mungu. Kila mtu aliye na upendo ni mtoto wa Mungu, na anamjua Mungu.

Sura   |  Matoleo
Wafilipi 1:3

Namshukuru Mungu wangu kila ninapowakumbukeni;

Sura   |  Matoleo
Wimbo Ulio Bora 2:4

Alinichukua hadi ukumbi wa karamu, akatweka bendera ya mapenzi juu yangu.

Sura   |  Matoleo
Waebrania 13:4

Ndoa inapaswa kuheshimiwa na watu wote, na haki zake zitekelezwe kwa uaminifu. Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi.

Sura   |  Matoleo
Wafilipi 2:2

Basi, ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na fikira moja, upendo mmoja, moyo mmoja na nia moja.

Sura   |  Matoleo
1 Wakorintho 7:3-5

Mume atimize wajibu alio nao kwa mkewe, naye mke atimize wajibu alio nao kwa mumewe.

wenye kulia wawe kama hawalii, na wenye kufurahi wawe kama hawafurahi; wanaonunua wawe kama hawana kitu;

nao wenye shughuli na dunia hii wawe kama vile hawana shughuli sana nayo. Maana ulimwengu huu, kama tuujuavyo, unapita.

Ningependa nyinyi msiwe na wasiwasi. Mtu asiye na mke hujishughulisha na kazi ya Bwana jinsi atakavyompendeza Bwana.

Mwanamume aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia jinsi atakavyompendeza mkewe,

naye amegawanyika. Mwanamke asiyeolewa au bikira hujishughulisha na mambo ya Bwana apate kujitolea mwili na roho kwa Bwana. Lakini mwanamke aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii jinsi atakavyompendeza mumewe.

Nawaambieni haya kwa faida yenu, na si kwa kuwawekeeni kizuizi. Nataka tu muwe na mpango unaofaa, mpate kumtumikia Bwana kwa moyo na nia moja.

Kama mtu anaona kwamba hamtendei vyema mchumba wake asipomwoa, na kama tamaa zake zinamshinda, na afanye atakavyo; waoane tu; hatakuwa ametenda dhambi.

Lakini kama huyo mwanamume akiamua kwa hiari moyoni mwake kutooa na kama anaweza kuzitawala tamaa zake na kuamua namna ya kufanya, basi, anafanya vizuri zaidi asipomwoa huyo mwenzake bikira.

Kwa maneno mengine: Yule anayeamua kuoa anafanya vema; naye anayeamua kutooa anafanya vema zaidi.

Mwanamke aliyeolewa huwa amefungwa na mumewe kwa muda wote mumewe aishipo. Lakini mumewe akifa, mama huyo yuko huru, na akipenda anaweza kuolewa na mtu yeyote, mradi tu iwe Kikristo.

Mke hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mumewe anayo; hali kadhalika naye mume, hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mkewe anayo.

Lakini, nionavyo mimi, atakuwa na heri zaidi kama akibaki hivyo alivyo. Hayo ni maoni yangu, na nafikiri mimi pia ninaye Roho wa Mungu.

Msinyimane haki zenu, isipokuwa kama mnaafikiana kufanya hivyo kwa kitambo tu, ili mpate nafasi nzuri ya kusali. Kisha rudianeni tena mara, ili Shetani asije akawajaribuni kwa sababu ya udhaifu wenu.

Sura   |  Matoleo
Waefeso 4:32

Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe nyinyi kwa njia ya Kristo.

Sura   |  Matoleo

Maombi kwa Mungu

Ee Mungu mwema wa milele, Bwana Mkuu, kwa jina la Yesu nakuja kwako, wewe pekee unastahili sifa kuu na kuabudiwa. Neno lako linasema: "Kwa maana mimi najua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho." Asante naweza kupumzika kwako, salama na kujiamini kama simba, hata katikati ya usiku mkuu, sitaogopa kwa sababu wewe ni nuru yangu na ngome yangu. Bwana, nisaidie nisiweke tumaini langu katika vitu vingine, bali kwako wewe pekee. Nashukuru kwa sababu umenifanya mwenye haki kwa neema yako, nakuomba unisaidie kuitunza daima ile tumaini la uzima wa milele moyoni mwangu, na kuilinda kwa hofu na tetemeko wokovu huu mkuu ulionipa. Nisaidie siku zote kuweka macho yangu juu, wala si katika vitu vya duniani, kwa maana uraia wangu uko mbinguni. Katika jina la Yesu. Amina!