Lakini BWANA akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza.
Methali 3:4 - Swahili Revised Union Version Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo utakubalika na kusifika, mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo utakubalika na kusifika, mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo utakubalika na kusifika, mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo utapata kibali na jina zuri mbele za Mungu na mwanadamu. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo utapata kibali na jina zuri mbele za Mungu na mwanadamu. BIBLIA KISWAHILI Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu. |
Lakini BWANA akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza.
Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri, Sifa zake zadumu milele.
wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu.
Naye BWANA akamwangalia Hana, naye akachukua mimba, akazaa watoto, watatu wa kiume na wawili wa kike. Naye huyo mtoto Samweli akakua mbele za BWANA.