Kisha Mefiboshethi, mwana wa Sauli, akashuka ili amlaki mfalme; alikuwa hakukata kucha za miguu yake wala kukata ndevu zake, wala kufua nguo zake, tangu siku alipoondoka mfalme, hadi siku hiyo aliporudi kwake kwa amani.
Methali 27:10 - Swahili Revised Union Version Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako, Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako. Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usisahau rafiki zako wala wa baba yako. Ukipatwa na janga usikimbilie kwa nduguyo; afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali. Biblia Habari Njema - BHND Usisahau rafiki zako wala wa baba yako. Ukipatwa na janga usikimbilie kwa nduguyo; afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usisahau rafiki zako wala wa baba yako. Ukipatwa na janga usikimbilie kwa nduguyo; afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali. Neno: Bibilia Takatifu Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako, tena usiende nyumbani mwa ndugu yako wakati umepatwa na maafa. Bora jirani wa karibu kuliko ndugu aliye mbali. Neno: Maandiko Matakatifu Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako, tena usiende nyumbani mwa ndugu yako wakati umepatwa na maafa. Bora jirani wa karibu kuliko ndugu aliye mbali. BIBLIA KISWAHILI Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako, Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako. Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali. |
Kisha Mefiboshethi, mwana wa Sauli, akashuka ili amlaki mfalme; alikuwa hakukata kucha za miguu yake wala kukata ndevu zake, wala kufua nguo zake, tangu siku alipoondoka mfalme, hadi siku hiyo aliporudi kwake kwa amani.
Kwa kuwa jamaa yote ya baba yangu walikuwa kama watu wa kufa tu mbele ya bwana wangu mfalme; ila uliniweka mimi mtumishi wako kati ya hao walao mezani pako. Basi ni haki gani sasa niliyo nayo, hata nimlilie mfalme zaidi?
Lakini mfalme akamwachilia Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha BWANA kilichokuwa kati yao, yaani, kati ya Daudi na Yonathani, mwana wa Sauli.
Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake Zekaria, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, BWANA na ayaangalie haya, akayalipie kisasi.
Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa maangamizi yake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.
Ndugu zote wa maskini humchukia; Jinsi gani rafiki zake huzidi kujitenga naye! Huwafuata kwa maneno, lakini wametoweka.
BWANA asema hivi, Baba zenu waliona dhuluma gani kwangu, hata wakafarakana nami, wakafuata ubatili, nao wakawa ubatili?
Kulipopambazuka, Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hadi wamwue Paulo.
Umwonapo ng'ombe wa nduguyo au kondoo wake akipotea, usijifiche kama usiyemwona; sharti utamrudisha kwa nduguyo.