Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.
Methali 24:16 - Swahili Revised Union Version Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema maana mtu mwema huanguka mara nyingi lakini huinuka, lakini mtu mwovu huangamizwa na janga. Biblia Habari Njema - BHND maana mtu mwema huanguka mara nyingi lakini huinuka, lakini mtu mwovu huangamizwa na janga. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza maana mtu mwema huanguka mara nyingi lakini huinuka, lakini mtu mwovu huangamizwa na janga. Neno: Bibilia Takatifu kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena; lakini waovu huangushwa chini na maafa. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena, lakini waovu huangushwa chini na maafa. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya. |
Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.
Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia.
Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai.
Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.
Nami nitawatawanya mbele ya adui, kama kwa upepo wa mashariki; nami nitaviangalia visogo vyao, wala si nyuso zao, siku ya msiba wao.
Tena utawaambia, BWANA asema hivi, Je! Watu wataanguka, wasisimame tena? Je! Mtu atageuka aende zake, asirudi tena?
Bwana MUNGU asema hivi; Ni jambo baya, jambo baya la namna ya peke yake; angalia, linakuja.
Bikira wa Israeli ameanguka; hatainuka tena; Ameangushwa katika nchi yake; hakuna mtu wa kumwinua.
Na hao waapao kwa dhambi ya Samaria, na kusema, Kama aishivyo Mungu wako, Ee Dani, na, Kama iishivyo njia ya Beer-sheba, hao nao wataanguka, wasiinuke tena.
Lakini kama hamtaki kufanya neno hilo, ninyi mmefanya dhambi mbele za BWANA, nanyi jueni ya kwamba hiyo dhambi yenu itawapata, hapana budi.
Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na wadudu, akatokwa na roho.
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
Daudi akasema, Aishivyo BWANA, BWANA atampiga; au siku yake ya kufa itampata; atashuka kwenda vitani na kupotea.
Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.