Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 32:23 - Swahili Revised Union Version

23 Lakini kama hamtaki kufanya neno hilo, ninyi mmefanya dhambi mbele za BWANA, nanyi jueni ya kwamba hiyo dhambi yenu itawapata, hapana budi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Lakini nawaonyeni kwamba msipotimiza ahadi yenu, mtakuwa mnamtendea Mwenyezi-Mungu dhambi; jueni kwa hakika kwamba mtaadhibiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Lakini nawaonyeni kwamba msipotimiza ahadi yenu, mtakuwa mnamtendea Mwenyezi-Mungu dhambi; jueni kwa hakika kwamba mtaadhibiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Lakini nawaonyeni kwamba msipotimiza ahadi yenu, mtakuwa mnamtendea Mwenyezi-Mungu dhambi; jueni kwa hakika kwamba mtaadhibiwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 “Lakini mkishindwa kufanya hili, mtakuwa mnatenda dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu; nanyi kuweni na hakika kuwa dhambi yenu itawapata.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 “Lakini mkishindwa kufanya hili, mtakuwa mnatenda dhambi dhidi ya bwana; nanyi kuweni na hakika kuwa dhambi yenu itawapata.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

23 Lakini kama hamtaki kufanya neno hilo, ninyi mmefanya dhambi mbele za BWANA, nanyi jueni ya kwamba hiyo dhambi yenu itawapata, hapana budi.

Tazama sura Nakili




Hesabu 32:23
21 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya BWANA.


Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, lakini yapasa uishinde.


Yuda akasema, Tumwambie nini bwana wangu? Tusemeje! Tujivutieje haki? Mungu ameona uovu wa watumwa wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, sisi na yeye ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake.


Nami leo nimedhoofika, hata nijapotiwa mafuta niwe mfalme; na watu hao, wana wa Seruya, ni wagumu kwangu mimi; BWANA amlipie mwovu kulingana na uovu wake.


Naye BWANA atamrudishia damu yake kichwani pake mwenyewe, kwa kuwa aliwapiga watu wawili wenye haki, na wema kuliko yeye, akawaua kwa upanga, wala babangu Daudi hakujua habari hiyo; yaani Abneri, mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli, na Amasa, mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la Yuda.


Hivyo damu yao itarudi kichwani pa Yoabu, na kichwani pa wazao wake hata milele; ila kwa Daudi, na kwa wazao wake, na kwa nyumba yake, na kwa kiti chake cha enzi, kutakuwa na amani hata milele kutoka kwa BWANA.


Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;


Msingiziaji hatawekwa imara katika nchi, Mtu wa jeuri, uovu humwinda kumwangamiza.


Umeyaweka maovu yetu mbele zako, Dhambi zetu za siri katika mwanga wa uso wako.


Uovu huwafuatia wenye dhambi; Bali mwenye haki atalipwa mema.


Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.


Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake.


Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa malipo ya mikono yake.


Maana makosa yetu yamezidi kuwa mengi mbele zako, na dhambi zetu zashuhudia juu yetu; maana makosa yetu tunayo pamoja nasi, na maovu yetu tumeyajua;


Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na tupige kura, tupate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona.


dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Mgiriki pia;


Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


Akawasongeza watu wa nyumba yake mmoja mmoja; na Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda akatwaliwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo