Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.
Methali 19:20 - Swahili Revised Union Version Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho, Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sikiliza shauri na kupokea mafundisho, upate hekima ya kukufaa siku zijazo. Biblia Habari Njema - BHND Sikiliza shauri na kupokea mafundisho, upate hekima ya kukufaa siku zijazo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sikiliza shauri na kupokea mafundisho, upate hekima ya kukufaa siku zijazo. Neno: Bibilia Takatifu Sikiliza mashauri na ukubali mafundisho, nawe mwishoni utakuwa na hekima. Neno: Maandiko Matakatifu Sikiliza mashauri na ukubali mafundisho, nawe mwishoni utakuwa na hekima. BIBLIA KISWAHILI Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho, Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho. |
Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.
Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.
Akataaye maonyo huidharau nafsi yake mwenyewe; Bali yeye asikilizaye lawama hujipatia ufahamu.
Uonyeke, Ee Yerusalemu, nafsi yangu, isije ikafarakana nawe; nisije nikakufanya ukiwa, nchi isiyokaliwa na watu.
Nilisema, Hakika utaniogopa, utakubali kurudiwa; ili yasikatiliwe mbali makao yake, sawasawa ya yote niliyoagiza katika habari zake; lakini waliondoka mapema na kuyaharibu matendo yao yote.
Ni nani awezaye kufanya idadi ya mavumbi ya Yakobo, Au kuhesabu robo ya Israeli? Na nife kifo chake mwenye haki, Na mwisho wangu uwe mfano wa mwisho wake.
aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako.