Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 23:10 - Swahili Revised Union Version

10 Ni nani awezaye kufanya idadi ya mavumbi ya Yakobo, Au kuhesabu robo ya Israeli? Na nife kifo chake mwenye haki, Na mwisho wangu uwe mfano wa mwisho wake.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Nani awezaye kuwahesabu wingi wa watu wa Yakobo, au kukisia umati wa Waisraeli? Nife kifo cha waadilifu, mwisho wangu na uwe kama wao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Nani awezaye kuwahesabu wingi wa watu wa Yakobo, au kukisia umati wa Waisraeli? Nife kifo cha waadilifu, mwisho wangu na uwe kama wao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Nani awezaye kuwahesabu wingi wa watu wa Yakobo, au kukisia umati wa Waisraeli? Nife kifo cha waadilifu, mwisho wangu na uwe kama wao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Ni nani awezaye kuhesabu mavumbi ya Yakobo, au kuhesabu robo ya Israeli? Mimi na nife kifo cha mtu mwenye haki, na mwisho wangu na uwe kama wao!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Ni nani awezaye kuhesabu mavumbi ya Yakobo, au kuhesabu robo ya Israeli? Mimi na nife kifo cha mtu mwenye haki, na mwisho wangu na uwe kama wao!”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Ni nani awezaye kufanya idadi ya mavumbi ya Yakobo, Au kuhesabu robo ya Israeli? Na nife kifo chake mwenye haki, Na mwisho wangu uwe mfano wa mwisho wake.

Tazama sura Nakili

Hesabu 23:10
20 Marejeleo ya Msalaba  

Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi; ikiwa mtu ataweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, uzao wako nao utahesabika.

katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao;

Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.

Kifo cha waaminifu wa Mungu, kina thamani machoni pa BWANA.

Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.

Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.

Wote waliohesabiwa katika kambi za Reubeni walikuwa elfu mia moja hamsini na moja na mia nne na hamsini, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaofuata wakiwa kundi la pili.

Wote waliohesabiwa katika kambi ya Efraimu walikuwa elfu mia moja na nane na mia moja, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaoondoka wakiwa kundi la tatu.

Wote waliohesabiwa katika kambi ya Dani walikuwa elfu mia moja hamsini na saba na mia sita. Hao ndio watakaoondoka mwisho kwa kufuata bendera yao.

Hao wote waliohesabiwa katika kambi ya Yuda walikuwa elfu mia moja themanini na sita na mia nne, kwa makundi yao. Hao ndio watakaotangulia mbele.

Nao wafalme wa Midiani wakawaua pamoja na watu wengine waliouawa; Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao wafalme watano wa Midiani; Balaamu mwana wa Beori naye wakamwua kwa upanga.

Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo