Sembuse yeye huwajali nyuso za wakuu, Wala hawajali matajiri kuliko maskini? Kwani wote ni kazi ya mikono yake,
Methali 18:5 - Swahili Revised Union Version Kukubali uso wake asiye haki si vizuri; Wala kumpotosha mwenye haki hukumuni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Si vizuri kumpendelea mtu mwovu, na kumnyima haki mtu mwadilifu. Biblia Habari Njema - BHND Si vizuri kumpendelea mtu mwovu, na kumnyima haki mtu mwadilifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Si vizuri kumpendelea mtu mwovu, na kumnyima haki mtu mwadilifu. Neno: Bibilia Takatifu Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu, au kumnyima haki asiye na hatia. Neno: Maandiko Matakatifu Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu, au kumnyima haki asiye na hatia. BIBLIA KISWAHILI Kukubali uso wake asiye haki si vizuri; Wala kumpotosha mwenye haki hukumuni. |
Sembuse yeye huwajali nyuso za wakuu, Wala hawajali matajiri kuliko maskini? Kwani wote ni kazi ya mikono yake,
Usiwafuate walio wengi kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu;
Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.
Na hukumu imegeuka ikaenda nyuma, na haki inasimama mbali sana; maana kweli imeanguka katika njia kuu, na unyofu hauwezi kuingia.
Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.
Sikieni haya, tafadhali, enyi vichwa vya nyumba ya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli, mnaochukia hukumu, na kuipotosha adili.
Mikono yao ni hodari kwa kutenda maovu; afisa na hakimu wanataka rushwa, mtu mkubwa hunena madhara yaliyomo rohoni mwake; hivyo ndivyo wayafumavyo hayo pamoja.
Wakatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodi, wakasema, Mwalimu, tunajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, na njia ya Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu awaye yote, kwa maana hutazami sura za watu.
Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza kesi wa wenye haki.