Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 17:15 - Swahili Revised Union Version

15 Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Kumsamehe mwenye hatia na kumwadhibu asiye na hatia yote mawili ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Kumsamehe mwenye hatia na kumwadhibu asiye na hatia yote mawili ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Kumsamehe mwenye hatia na kumwadhibu asiye na hatia yote mawili ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Yeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki, naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki: Mwenyezi Mungu huwachukia sana wote wawili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Yeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki, naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki: bwana huwachukia sana wote wawili.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.

Tazama sura Nakili




Methali 17:15
23 Marejeleo ya Msalaba  

Na hao watu wawili, watu wasiofaa, wakaingia, wakaketi mbele yake; wale watu wasiofaa wakamshuhudia Nabothi mbele ya watu, wakasema, Nabothi amemtukana Mungu na mfalme. Ndipo wakamchukua nje ya mji, wakampiga kwa mawe hata akafa.


Kwa pamoja wanaishambulia nafsi yake mwenye haki, Na kuihukumu damu isiyo na hatia.


Jitenge mbali na neno la uongo; wala wasio hatia na wenye haki usiwaue; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu.


Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza.


Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.


Tena kumwadhibu mwenye haki si vizuri; Wala si vyema kuwapiga wakuu kwa unyofu wao.


Kukubali uso wake asiye haki si vizuri; Wala kumpotosha mwenye haki hukumuni.


Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.


Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.


Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!


wampao haki mwenye uovu, ili wapewe ijara, na kumwondolea mwenye haki haki yake!


Kuipotosha hukumu ya mtu Mbele zake Aliye Juu,


Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.


Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa; ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao.


Ninyi mnaogeuza hukumu kuwa uchungu, na kuiangusha haki chini,


Je! Farasi watapiga mbio juu ya mwamba? Je! Mtu atalima kwa plau na ng'ombe baharini? Hata mmegeuza hukumu kuwa sumu, na matunda ya haki kuwa uchungu;


Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.


Pakiwa na mashindano kati ya watu, wakaenda maamuzini, na hao waamuzi wakawaamua; na wampe haki mwenye haki, na wamhukumie makosa yule mwovu;


Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo