Ikawa, Ahabu alipomwona Eliya, Ahabu akamwambia, Je! Ni wewe, Ewe mtaabishaji wa Israeli?
Methali 15:10 - Swahili Revised Union Version Adhabu kali ina yeye aiachaye njia; Naye achukiaye kukemewa atakufa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Adhabu kali ipo kwa wanaoacha mwenendo mwema; yeyote achukiaye kuonywa atakufa. Biblia Habari Njema - BHND Adhabu kali ipo kwa wanaoacha mwenendo mwema; yeyote achukiaye kuonywa atakufa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Adhabu kali ipo kwa wanaoacha mwenendo mwema; yeyote achukiaye kuonywa atakufa. Neno: Bibilia Takatifu Adhabu kali humngoja yeye aachaye njia; yeye achukiaye maonyo atakufa. Neno: Maandiko Matakatifu Adhabu kali humngoja yeye aachaye njia; yeye achukiaye maonyo atakufa. BIBLIA KISWAHILI Adhabu kali ina yeye aiachaye njia; Naye achukiaye kukemewa atakufa. |
Ikawa, Ahabu alipomwona Eliya, Ahabu akamwambia, Je! Ni wewe, Ewe mtaabishaji wa Israeli?
Ahabu akamwambia Eliya, Je! Umenipata, ewe adui yangu? Akamwambia, Nimekupata, kwa sababu umejiuza utende yaliyo mabaya machoni pa BWANA.
Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Yupo mtu mmoja, ambaye tungeweza kumwuliza BWANA kwa yeye, yaani Mikaya mwana wa Imla; lakini namchukia; kwa sababu hanibashirii mema, ila mabaya. Yehoshafati akasema, La! Mfalme asiseme hivi.
Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
Je! Hukujipatia mambo haya mwenyewe, kwa kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, alipokuongoza njiani?
Lakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako.
Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.
Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.