Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Abrahamu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu.
Methali 14:26 - Swahili Revised Union Version Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amchaye Mwenyezi-Mungu ana tumaini imara, na watoto wake watapata kimbilio salama. Biblia Habari Njema - BHND Amchaye Mwenyezi-Mungu ana tumaini imara, na watoto wake watapata kimbilio salama. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amchaye Mwenyezi-Mungu ana tumaini imara, na watoto wake watapata kimbilio salama. Neno: Bibilia Takatifu Yeye amchaye Mwenyezi Mungu ana ngome salama, na kwa watoto wake itakuwa kimbilio. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye amchaye bwana ana ngome salama, na kwa watoto wake itakuwa kimbilio. BIBLIA KISWAHILI Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio. |
Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Abrahamu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu.
Ni vizuri kwamba ulishike neno hilo; naam, hata kwa neno hilo tena usiuondoe mkono wako; kwa kuwa mtu yule amchaye Mungu atatoka katika hayo yote.
Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba.
BWANA akasema, Hakika nitakutia nguvu upate mema; hakika nitamlazimisha adui akusihi wakati wa uovu, na wakati wa taabu.
Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawachomozea, likiwa na uwezo wa kuponya katika miale yake; nanyi mtatoka nje, na kuchezacheza kama ndama watokapo mazizini.
Basi kanisa likapata raha kote katika Yudea na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.