Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.
Methali 13:18 - Swahili Revised Union Version Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa; Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Umaskini na fedheha humpata asiyejali mafundisho, lakini mwenye kusikia maonyo huheshimiwa. Biblia Habari Njema - BHND Umaskini na fedheha humpata asiyejali mafundisho, lakini mwenye kusikia maonyo huheshimiwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Umaskini na fedheha humpata asiyejali mafundisho, lakini mwenye kusikia maonyo huheshimiwa. Neno: Bibilia Takatifu Yeye anayedharau maonyo hupata umaskini na aibu, bali yeye anayekubali maonyo huheshimiwa. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye anayedharau maonyo hupata umaskini na aibu, bali yeye anayekubali maonyo huheshimiwa. BIBLIA KISWAHILI Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa; Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa. |
Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.
Kila anayelidharau neno hujiletea uharibifu; Bali yeye anayeiogopa amri atapewa thawabu.
Haja iliyopatikana ni tamu nafsini mwa mtu; Bali kujitenga na maovu ni chukizo kwa wapumbavu.
Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.
Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;
Na tulale kwa aibu yetu, haya yetu na itufunike; kwa maana tumemwasi BWANA, Mungu wetu, sisi na baba zetu, tangu ujana wetu hata leo; wala hatukuitii sauti ya BWANA, Mungu wetu.
Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni;