BWANA alinitendea kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu akanilipa.
Methali 11:31 - Swahili Revised Union Version Ikiwa, mwenye haki atalipwa duniani; Je, mwovu na mkosaji hawatalipwa mara nyingi zaidi? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ikiwa mwadilifu hupata tuzo hapa duniani, hakika mwovu na mwenye dhambi atapatilizwa. Biblia Habari Njema - BHND Ikiwa mwadilifu hupata tuzo hapa duniani, hakika mwovu na mwenye dhambi atapatilizwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ikiwa mwadilifu hupata tuzo hapa duniani, hakika mwovu na mwenye dhambi atapatilizwa. Neno: Bibilia Takatifu Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani, si zaidi sana mtu asiyemcha Mungu, na mwenye dhambi? Neno: Maandiko Matakatifu Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani, si zaidi sana yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi? BIBLIA KISWAHILI Ikiwa, mwenye haki atalipwa duniani; Je, mwovu na mkosaji hawatalipwa mara nyingi zaidi? |
BWANA alinitendea kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu akanilipa.
Basi BWANA amenilipa kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu mbele zake.
Na alipokuwa amekwenda zake, simba alimkuta njiani, akamwua. Maiti yake ikatupwa njiani, na yule punda akasimama karibu naye; na yule simba naye akasimama karibu na maiti.
Fundi stadi hufanyiza vitu vyote; Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao.
Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayashusha chini majivuno yao walio wakali;
Maana angalieni, ninaanza kutenda mabaya katika mji uitwao kwa jina langu, je! Mtaachiliwa ninyi msiadhibiwe? Hamtaachiliwa msiadhibiwe; kwa maana nitauita upanga ule uwapige wote wakaao katika dunia, asema BWANA wa majeshi.
Lakini Walawi waliofarakana nami, wakapotea na kuvifuata vinyago vyao, hapo Waisraeli walipopotea, watachukua uovu wao wenyewe.
Hata itakuwa, kama walivyo watu, ndivyo atakavyokuwa kuhani; nami nitawaadhibu kwa ajili ya njia zao, na kuwalipa kwa matendo yao.