Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 11:31 - Swahili Revised Union Version

31 Ikiwa, mwenye haki atalipwa duniani; Je, mwovu na mkosaji hawatalipwa mara nyingi zaidi?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Ikiwa mwadilifu hupata tuzo hapa duniani, hakika mwovu na mwenye dhambi atapatilizwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Ikiwa mwadilifu hupata tuzo hapa duniani, hakika mwovu na mwenye dhambi atapatilizwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Ikiwa mwadilifu hupata tuzo hapa duniani, hakika mwovu na mwenye dhambi atapatilizwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani, si zaidi sana mtu asiyemcha Mungu, na mwenye dhambi?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani, si zaidi sana yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

31 Ikiwa, mwenye haki atalipwa duniani; Je, mwovu na mkosaji hawatalipwa mara nyingi zaidi?

Tazama sura Nakili




Methali 11:31
15 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA alinitendea kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu akanilipa.


Basi BWANA amenilipa kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu mbele zake.


Na alipokuwa amekwenda zake, simba alimkuta njiani, akamwua. Maiti yake ikatupwa njiani, na yule punda akasimama karibu naye; na yule simba naye akasimama karibu na maiti.


Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama.


Uovu huwafuatia wenye dhambi; Bali mwenye haki atalipwa mema.


Fundi stadi hufanyiza vitu vyote; Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao.


Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayashusha chini majivuno yao walio wakali;


Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa malipo ya mikono yake.


Maana angalieni, ninaanza kutenda mabaya katika mji uitwao kwa jina langu, je! Mtaachiliwa ninyi msiadhibiwe? Hamtaachiliwa msiadhibiwe; kwa maana nitauita upanga ule uwapige wote wakaao katika dunia, asema BWANA wa majeshi.


Lakini Walawi waliofarakana nami, wakapotea na kuvifuata vinyago vyao, hapo Waisraeli walipopotea, watachukua uovu wao wenyewe.


Hata itakuwa, kama walivyo watu, ndivyo atakavyokuwa kuhani; nami nitawaadhibu kwa ajili ya njia zao, na kuwalipa kwa matendo yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo