nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
Methali 10:22 - Swahili Revised Union Version Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baraka za Mwenyezi-Mungu ndizo ziletazo fanaka, juhudi za mtu haziongezi hapo chochote. Biblia Habari Njema - BHND Baraka za Mwenyezi-Mungu ndizo ziletazo fanaka, juhudi za mtu haziongezi hapo chochote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baraka za Mwenyezi-Mungu ndizo ziletazo fanaka, juhudi za mtu haziongezi hapo chochote. Neno: Bibilia Takatifu Baraka ya Mwenyezi Mungu hutajirisha, wala haichanganyi na huzuni. Neno: Maandiko Matakatifu Baraka ya bwana hutajirisha, wala haichanganyi huzuni. BIBLIA KISWAHILI Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo. |
nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala chochote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu;
na BWANA amembarikia sana bwana wangu, amekuwa mtu mkuu; amempa kondoo, na ng'ombe, na fedha, na dhahabu, na watumishi, na wajakazi, na ngamia, na punda.
Mwaka huo Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, naye akapata mavuno mara mia zaidi. BWANA akambariki.
Ukamwambie, ukisema, BWANA asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, BWANA asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.
Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibariki kweli kweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
Amazia akamwambia mtu wa Mungu, Lakini tuzifanyieje zile talanta mia moja nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, BWANA aweza kukupa zaidi sana kuliko hizo.
Naye Hezekia akawa na mali nyingi mno na heshima; akajitengenezea hazina za fedha, za dhahabu, za vito, za manukato, za ngao, na za namna zote za vyombo vya thamani;
Tena akajitengenezea miji, na mali za kondoo na ng'ombe kwa wingi; maana Mungu alimtajirisha sana sana.
Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme.
Nitaituma itokee, asema BWANA wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi, na katika nyumba ya yeyote aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katika nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.
Na sasa, tazama, nimeleta malimbuko ya mazao ya ardhi uliyonipa, Ee BWANA. Kisha ukiweke chini mbele za BWANA, Mungu wako, ukasujudu mbele za BWANA, Mungu wako;
BWANA atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako kwamba atakupa.
Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu; msije mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo mtaifanya kambi ya Israeli kuwa imelaaniwa na kuifadhaisha.