Mathayo 26:49 - Swahili Revised Union Version Mara akamwendea Yesu, akasema, Salamu, Rabi, akambusu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Yuda akamkaribia Yesu, akamwambia, “Shikamoo, Mwalimu!” Kisha akambusu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Yuda akamkaribia Yesu, akamwambia, “Shikamoo, Mwalimu!” Kisha akambusu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Yuda akamkaribia Yesu, akamwambia, “Shikamoo, Mwalimu!” Kisha akambusu. Neno: Bibilia Takatifu Mara Yuda akamjia Isa na kumsalimu, “Salamu, Mwalimu!” Akambusu. Neno: Maandiko Matakatifu Mara Yuda akamjia Isa na kumsalimu, “Salamu, Mwalimu!” Akambusu. BIBLIA KISWAHILI Mara akamwendea Yesu, akasema, Salamu, Rabi, akambusu. |
Naye Yoabu akamwambia Amasa, Amani kwako, ndugu yangu. Kisha Yoabu akamshika Amasa ndevu kwa mkono wake wa kulia ili ambusu.
Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni.
Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! BWANA hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa kutoka kwa mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake.