Wakaniambia, Watu waliosalimika, waliosalia huko katika mkoa ule, wamo katika hali ya dhiki kubwa na aibu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Maombolezo 5:1 - Swahili Revised Union Version Ee BWANA, kumbuka yaliyotupata; Utazame na kuiona aibu yetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ukumbuke ee Mwenyezi-Mungu, mambo yaliyotupata! Utuangalie, uone jinsi tulivyoaibishwa! Biblia Habari Njema - BHND Ukumbuke ee Mwenyezi-Mungu, mambo yaliyotupata! Utuangalie, uone jinsi tulivyoaibishwa! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ukumbuke ee Mwenyezi-Mungu, mambo yaliyotupata! Utuangalie, uone jinsi tulivyoaibishwa! Neno: Bibilia Takatifu Kumbuka, Ee Mwenyezi Mungu, yaliyotupata, tazama, nawe uione aibu yetu. Neno: Maandiko Matakatifu Kumbuka, Ee bwana, yaliyotupata, tazama, nawe uione aibu yetu. BIBLIA KISWAHILI Ee BWANA, kumbuka yaliyotupata; Utazame na kuiona aibu yetu. |
Wakaniambia, Watu waliosalimika, waliosalia huko katika mkoa ule, wamo katika hali ya dhiki kubwa na aibu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.
Nakuomba, likumbuke neno lile ulilomwamuru Musa, mtumishi wako, ukisema, Mkikosa, nitawatawanya kati ya mataifa;
Sikia, Ee Mungu wetu; maana tunadharauliwa; ukawarudishie mashutumu yao juu ya vichwa vyao, ukawatoe watekwe katika nchi ya uhamisho;
Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo; Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?
Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya;
Ee BWANA, unajua wewe; unikumbuke, unijie, ukanilipizie kisasi juu yao wanaoniudhi; usiniondoe kwa uvumilivu wako; ujue ya kuwa ni kwa ajili yako nilivyopatikana na matukano.
Twaona haya kwa kuwa tumesikia shutuma; Fedheha imetufunika nyuso zetu; Kwa sababu wageni wamepaingia Patakatifu pa nyumba ya BWANA.
Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamanio yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge.
Angalia, Ee BWANA; maana mimi ni katika dhiki; Mtima wangu umetaabika; Moyo wangu umegeuka ndani yangu; Maana nimeasi vibaya sana; Huko nje upanga huua watu; Nyumbani mna kama mauti.
Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, BWANA, mateso yangu; Maana huyo adui amejitukuza.
Hao watu wote wapitao Hukupigia makofi; Humzomea binti Yerusalemu, Na kutikisa vichwa vyao; Je! Mji huu ndio ulioitwa, Ukamilifu wa uzuri, Furaha ya dunia yote?
Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana?
Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema.