Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Maombolezo 1:20 - Swahili Revised Union Version

20 Angalia, Ee BWANA; maana mimi ni katika dhiki; Mtima wangu umetaabika; Moyo wangu umegeuka ndani yangu; Maana nimeasi vibaya sana; Huko nje upanga huua watu; Nyumbani mna kama mauti.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 “Ona, ee Mwenyezi-Mungu nilivyo taabuni. Roho yangu imechafuka, moyo wangu unasononeka kwani nimekuasi vibaya. Huko nje kumejaa mauaji, ndani nako ni kama kifo tu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 “Ona, ee Mwenyezi-Mungu nilivyo taabuni. Roho yangu imechafuka, moyo wangu unasononeka kwani nimekuasi vibaya. Huko nje kumejaa mauaji, ndani nako ni kama kifo tu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 “Ona, ee Mwenyezi-Mungu nilivyo taabuni. Roho yangu imechafuka, moyo wangu unasononeka kwani nimekuasi vibaya. Huko nje kumejaa mauaji, ndani nako ni kama kifo tu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 “Angalia, Ee Mwenyezi Mungu, jinsi nilivyo katika dhiki! Nina maumivu makali ndani yangu, nami ninahangaika moyoni mwangu, kwa kuwa nimekuwa mwasi sana. Huko nje, upanga unaua watu, ndani, kipo kifo tu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 “Angalia, Ee bwana, jinsi nilivyo katika dhiki! Nina maumivu makali ndani yangu, nami ninahangaika moyoni mwangu, kwa kuwa nimekuwa mwasi sana. Huko nje, upanga unaua watu, ndani, kipo kifo tu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

20 Angalia, Ee BWANA; maana mimi ni katika dhiki; Mtima wangu umetaabika; Moyo wangu umegeuka ndani yangu; Maana nimeasi vibaya sana; Huko nje upanga huua watu; Nyumbani mna kama mauti.

Tazama sura Nakili




Maombolezo 1:20
32 Marejeleo ya Msalaba  

Matumbo yangu yatokota, wala hayaachi; Siku za taabu zimenijia.


Yeye huimba mbele ya watu, na kusema, Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea, Wala sikulipizwa jambo hilo;


Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya moyo wangu.


Nimedhoofika na kupondeka sana, Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu.


Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.


Kwa sababu hiyo mtima wangu unamlilia Moabu kama kinubi, na nafsi yangu kwa ajili ya Kir-Heresi.


Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Niliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.


Nikitoka kwenda shambani, tazama, wako huko waliouawa kwa upanga! Na nikiingia mjini, tazama, wamo humo wanaougua kwa sababu ya njaa! Maana nabii na kuhani, wote wawili, huenda huku na huko katika nchi, wala hawana maarifa.


Ee BWANA, tunakiri uovu wetu, na ubaya wa baba zetu; maana tumekutenda dhambi.


Lakini ulisema, Sina hatia mimi; bila shaka hasira yake imegeuka na kuniacha. Tazama, nitaingia hukumuni pamoja nawe, kwa sababu unasema, Sikutenda dhambi mimi.


Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi BWANA, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi, wala hamkuitii sauti yangu, asema BWANA.


Je! Efraimu siye mwanangu mpendwa? Je! Siye mtoto apendezaye? Maana kila nisemapo neno juu yake, ningali nikimkumbuka sana; kwa sababu hiyo moyo wangu unataabika kwa ajili yake; bila shaka nitamrehemu, asema BWANA.


Mtima wangu, mtima wangu! Naumwa katika moyo wangu wa ndani; moyo wangu umefadhaika ndani yangu; siwezi kunyamaza; kwa sababu umesikia, Ee nafsi yangu, sauti ya tarumbeta, mshindo wa vita.


Kwa sababu hiyo moyo wangu watoa sauti kama filimbi kwa ajili ya Moabu, na kwa ajili ya watu wa Kir-heresi, moyo wangu watoa sauti kama filimbi; kwa kuwa wingi aliojipatia umepotea.


Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamanio yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge.


BWANA ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka.


Yerusalemu amefanya dhambi sana; Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu; Wote waliomheshimu wanamdharau, Kwa sababu wameuona uchi wake; Naam, yeye anaugua, Na kujigeuza aende nyuma.


Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, BWANA, mateso yangu; Maana huyo adui amejitukuza.


Macho yangu yamechoka kwa machozi, Mtima wangu umetaabika; Ini langu linamiminwa juu ya nchi Kwa uharibifu wa binti ya watu wangu; Kwa sababu watoto wachanga na wanyonyao, Huzimia katika mitaa ya mji.


Taji ya kichwa chetu imeanguka; Ole wetu! Kwa kuwa tumetenda dhambi.


Upanga uko nje, na tauni na njaa zimo ndani; yeye aliye nje mashambani atakufa kwa upanga; na yeye aliye ndani ya mji, njaa na tauni zitamla.


tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako;


Niwezeje kukuacha, Efraimu? Niwezeje kukuachilia Israeli? Niwezeje kukufanya kama Adma? Niwezeje kukuweka kama Seboimu? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zimewaka pamoja.


Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.


Nje upanga utawafifiliza Na ndani ya vyumba, utisho; Utaangamiza mvulana na msichana, Anyonyaye pamoja na mwenye mvi,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo