Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Maombolezo 5:1 - Swahili Revised Union Version

1 Ee BWANA, kumbuka yaliyotupata; Utazame na kuiona aibu yetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Ukumbuke ee Mwenyezi-Mungu, mambo yaliyotupata! Utuangalie, uone jinsi tulivyoaibishwa!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Ukumbuke ee Mwenyezi-Mungu, mambo yaliyotupata! Utuangalie, uone jinsi tulivyoaibishwa!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Ukumbuke ee Mwenyezi-Mungu, mambo yaliyotupata! Utuangalie, uone jinsi tulivyoaibishwa!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kumbuka, Ee Mwenyezi Mungu, yaliyotupata, tazama, nawe uione aibu yetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kumbuka, Ee bwana, yaliyotupata, tazama, nawe uione aibu yetu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Ee BWANA, kumbuka yaliyotupata; Utazame na kuiona aibu yetu.

Tazama sura Nakili




Maombolezo 5:1
26 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaniambia, Watu waliosalimika, waliosalia huko katika mkoa ule, wamo katika hali ya dhiki kubwa na aibu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.


Nakuomba, likumbuke neno lile ulilomwamuru Musa, mtumishi wako, ukisema, Mkikosa, nitawatawanya kati ya mataifa;


Sikia, Ee Mungu wetu; maana tunadharauliwa; ukawarudishie mashutumu yao juu ya vichwa vyao, ukawatoe watekwe katika nchi ya uhamisho;


Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo; Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?


Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo; Jicho langu halitaona mema tena.


Uyaangalie mateso yangu, uniokoe, Maana sikuisahau sheria yako.


Ee BWANA, uyakumbuke hayo, adui amelaumu, Na watu wapumbavu wamelidharau jina lako.


Uwalipe jirani zetu mara saba vifuani mwao Laumu zao walizokulaumu, Ee Bwana.


Tumekuwa lawama kwa jirani zetu, Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.


Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya;


Ee BWANA, unajua wewe; unikumbuke, unijie, ukanilipizie kisasi juu yao wanaoniudhi; usiniondoe kwa uvumilivu wako; ujue ya kuwa ni kwa ajili yako nilivyopatikana na matukano.


Twaona haya kwa kuwa tumesikia shutuma; Fedheha imetufunika nyuso zetu; Kwa sababu wageni wamepaingia Patakatifu pa nyumba ya BWANA.


Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamanio yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge.


Angalia, Ee BWANA; maana mimi ni katika dhiki; Mtima wangu umetaabika; Moyo wangu umegeuka ndani yangu; Maana nimeasi vibaya sana; Huko nje upanga huua watu; Nyumbani mna kama mauti.


Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake; Hakukumbuka mwisho wake; Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu; Yeye hana mtu wa kumfariji; Tazama, BWANA, mateso yangu; Maana huyo adui amejitukuza.


Hao watu wote wapitao Hukupigia makofi; Humzomea binti Yerusalemu, Na kutikisa vichwa vyao; Je! Mji huu ndio ulioitwa, Ukamilifu wa uzuri, Furaha ya dunia yote?


Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana?


Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu, Pakanga na nyongo.


Hata BWANA atakapoangalia Na kutazama toka mbinguni.


Ee BWANA, umeyasikia matukano yao, Na mashauri yao yote juu yangu;


Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema.


Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo