Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Maombolezo 2:20 - Swahili Revised Union Version

20 Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Tazama ee Mwenyezi-Mungu uone! Je, kuna yeyote uliyemtendea ulivyotutendea sisi? Je, hata kina mama wawale watoto wao? Je, nao makuhani wauawe hekaluni mwako?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Tazama ee Mwenyezi-Mungu uone! Je, kuna yeyote uliyemtendea ulivyotutendea sisi? Je, hata kina mama wawale watoto wao? Je, nao makuhani wauawe hekaluni mwako?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Tazama ee Mwenyezi-Mungu uone! Je, kuna yeyote uliyemtendea ulivyotutendea sisi? Je, hata kina mama wawale watoto wao? Je, nao makuhani wauawe hekaluni mwako?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 “Tazama, Ee Mwenyezi Mungu, ufikirie: Ni nani ambaye umepata kumtendea namna hii? Je, wanawake wale wazao wao, watoto waliowalea? Je, kuhani na nabii auawe mahali patakatifu pa Bwana?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 “Tazama, Ee bwana, ufikirie: Ni nani ambaye umepata kumtendea namna hii? Je, wanawake wakule wazao wao, watoto waliowalea? Je, kuhani na nabii auawe mahali patakatifu pa Bwana?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

20 Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana?

Tazama sura Nakili




Maombolezo 2:20
24 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mnyonge; akawatia wote mkononi mwake.


Makuhani wao walianguka kwa upanga, Wala wajane wao hawakuomboleza.


Musa akamsihi sana BWANA, Mungu wake, na kusema, BWANA, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?


Ewe uliyejaa makelele, Mji wa ghasia, mji wenye furaha; Watu wako waliouawa hawakuuawa kwa upanga, Wala hawakufa vitani.


Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawatesa.


Na baada ya hayo, asema BWANA, nitamtia Sedekia, mfalme wa Yuda, na watumishi wake, na watu wote waliosalia ndani ya mji huu, baada ya tauni ile, na upanga, na njaa, katika mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao; naye atawaua kwa ukali wa upanga; hatawaachilia, wala hatawahurumia, wala hatawarehemu.


Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?


Niliwaita hao walionipenda Lakini walinidanganya; Makuhani wangu na wazee wangu Walifariki mjini; Hapo walipokuwa wakitafuta chakula ili kuzihuisha nafsi zao.


Mikono ya wanawake wenye huruma Imewatokosa watoto wao wenyewe; Walikuwa ndio chakula chao Katika uharibifu wa binti ya watu wangu.


Ni kwa sababu ya dhambi za manabii wake Na maovu ya makuhani wake, Walioimwaga damu ya wenye haki Katikati yake.


Hasira ya BWANA imewatenga, Yeye hatawaangalia tena; Hawakujali nafsi za wale makuhani, Hawakuwaheshimu wazee wao.


Kwa sababu hiyo baba za watu watawala wana wao kati yako, nao wana watawala baba zao; nami nitafanya hukumu ndani yako, na hao wote waliosalia kwako nitawatawanya kwa pepo zote.


Akawaambia, itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa; haya, nendeni. Wakaenenda, wakaua watu katika mji.


Nanyi mtakula nyama ya miili ya watoto wenu wa kiume, na nyama ya miili ya binti zenu mtaila.


Nikamwomba BWANA, nikasema, Ee Bwana Mungu, usiwaangamize watu wako, urithi wako, uliowakomboa kwa ukuu wako, uliowatoa Misri kwa mkono wa nguvu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo