Ee Mwenyezi-Mungu, alfajiri waisikia sauti yangu, asubuhi nakutolea tambiko yangu, kisha nangojea unijibu.
Naamka kabla ya pambazuko na kukuomba msaada; naweka tumaini langu katika maneno yako.
Ee Mungu, wewe u Mungu wangu, nami nakutafuta kwa moyo; roho yangu inakutamani kama mtu mwenye kiu; nina kiu kama nchi kavu isiyo na maji.
Ninamtumainia Mwenyezi-Mungu kuliko walinzi wanavyongojea pambazuko; kuliko walinzi wanavyongojea kuche asubuhi.
Moyo wangu wakutamani usiku kucha, nafsi yangu yakutafuta kwa moyo. Utakapoihukumu dunia, watu wote ulimwenguni watajifunza haki.
Ee Mungu mtetezi wa haki yangu, unijibu niombapo. Nilipokuwa katika shida, wewe ulinisaidia; unionee huruma na kusikia sala yangu.
Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango, kisha umwombe Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.
Kama paa atamanivyo maji ya kijito, ndivyo ninavyokutamani, ee Mungu wangu! Nimepondwa kwa matukano yao, wanaponiuliza kila siku: “Yuko wapi, Mungu wako!” Mbona nasononeka hivyo moyoni? Kwa nini nahangaika hivyo? Nitamtumainia Mungu, maana nitamsifu tena Mungu, aliye msaada wangu na Mungu wangu. Naona kiu ya Mungu, kiu ya Mungu aliye hai. Nitafika lini kwake na kuuona uso wake?
Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi, huruma zake hazina mwisho. Kila kunapokucha ni mpya kabisa, uaminifu wake ni mkuu mno.
Basi, na tukikaribie bila hofu kiti cha enzi cha Mungu mwenye neema, tupokee huruma na neema ya kutusaidia wakati wa shida.
Uniongoze katika ukweli wako na kunifundisha, kwani wewe ni Mungu, mwokozi wangu; ninakutegemea wewe kila siku.
Nakulilia kwa moyo wangu wote; unijibu, ee Mwenyezi-Mungu, nifuate kanuni zako. Nakulilia, unisalimishe; nipate kuyazingatia maamuzi yako.
Msiwe na wasiwasi juu ya kitu chochote, ila kwa kila hali, mwombeni Mungu katika sala juu ya mahitaji yenu, kwa shukrani. Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote za watu italinda salama mioyo na akili zenu katika kuungana na Kristo Yesu.
Tulia mbele ya Mwenyezi-Mungu, mngojee kwa saburi; usihangaike juu ya wale wanaofanikiwa, watu wanaofaulu katika mipango yao mibaya.
Roho yangu inafurahi kama kwa karamu na vinono; kwa shangwe nitaimba sifa zako. Niwapo kitandani ninakukumbuka, usiku kucha ninakufikiria;
Bwana Mungu amenipa ufasaha wa lugha, niwatie moyo wale waliochoka. Kila asubuhi hunipa hamu ya kusikiliza anayotaka kunifunza.
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Heri mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, anayefurahia sana kutii amri zake.
Kila mara ninapokuomba msaada wako, maadui zangu wanarudishwa nyuma. Najua kweli Mungu yuko upande wangu.
Lakini mimi nakutumainia wewe, ee Mwenyezi-Mungu. Nasema: “Wewe ni Mungu wangu!” Maisha yangu yamo mikononi mwako; uniokoe na maadui zangu, niokoe na hao wanaonidhulumu.
Ndipo mtakapoomba, nami Mwenyezi-Mungu nitawaitikia; mtalia kwa sauti kuomba msaada, nami nitajibu, ‘Niko hapa!’ “Kama mkiiondoa dhuluma kati yenu, mkiacha kudharau wengine na kusema maovu,
Lakini ninakutumainia wewe, ee Mwenyezi-Mungu; wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, ndiwe utakayenijibu.
Sadaka ya waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini sala ya wanyofu humfurahisha Mungu.
Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida, na kusali daima.
Lakini, kwangu ni vema kuwa karibu na Mungu, wewe Bwana Mwenyezi-Mungu ndiwe usalama wangu. Nitatangaza mambo yote uliyotenda!
Basi, usiogope, mimi nipo pamoja nawe. Usifadhaike, mimi ni Mungu wako. Nitakuimarisha na kukusaidia; nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi.
Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umenichunguza; wewe wanijua mpaka ndani. hata huko upo kuniongoza; mkono wako wa kulia utanitegemeza. Kama ningeliomba giza linifunike, giza linizunguke badala ya mwanga, kwako giza si giza hata kidogo, na usiku wangaa kama mchana; kwako giza na mwanga ni mamoja. Wewe umeniumba, mwili wangu wote; ulinitengeneza tumboni mwa mama yangu. Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako ni ya ajabu; wewe wanijua kabisakabisa. Umbo langu halikufichika kwako nilipotungwa kwa siri na ustadi ndani ya dunia. Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa, uliandika kila kitu kitabuni mwako; siku zangu zote ulizipanga, hata kabla ya kuweko ile ya kwanza. Ee Mungu, mawazo yako ni makuu mno; hayawezi kabisa kuhesabika. Ningeyahesabu yangekuwa mengi kuliko mchanga. Niamkapo, bado nipo pamoja nawe. Laiti, ee Mungu, ungewaua watu waovu! Laiti watu wauaji wangeondoka kwangu! Nikiketi au nikisimama, wewe wajua; wajua kutoka mbali kila kitu ninachofikiria.
Hatimaye, ndugu zangu, zingatieni mambo mema na yanayostahili kusifiwa; mambo ya kweli na bora; mambo ya haki, safi, ya kupendeza na ya heshima.
Namtumainia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote; nina imani sana na neno lake. Ninamtumainia Mwenyezi-Mungu kuliko walinzi wanavyongojea pambazuko; kuliko walinzi wanavyongojea kuche asubuhi.
Ee Mungu Mkuu, hofu inaponishika, mimi nakutumainia wewe. Namtumainia Mungu na kusifu neno lake; namtumainia Mungu, wala siogopi. Binadamu dhaifu atanifanya nini?
Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima; wote wanaozitii amri zake hujaliwa busara. Sifa zake zadumu milele.
Ee Mungu, wawaweka katika amani walio thabiti, wawaweka katika amani kwa kuwa wanakutegemea. Mtumaini Mwenyezi-Mungu siku zote kwa maana yeye ni mwamba wa usalama milele.
Niwapo kitandani ninakukumbuka, usiku kucha ninakufikiria; maana wewe umenisaidia daima. Kivulini mwa mabawa yako nitashangilia.
Maana wewe Mwenyezi-Mungu wawabariki waadilifu; wawakinga kwa fadhili zako kama kwa ngao.
Mwenyezi-Mungu atanijalia fadhili zake mchana; nami nimwimbie wimbo wa sifa usiku, nimwombe Mungu anipaye uhai.
Nafsi yangu yatamani mno maskani ya Mwenyezi-Mungu! Moyo na mwili wangu wote wamshangilia Mungu aliye hai.
Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu, watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea.
Unichunguze, ee Mungu, unijue moyo wangu, unipime, uyajue mawazo yangu. Uangalie kama mwenendo wangu ni mbaya, uniongoze katika njia ya milele.
Hali kadhalika, naye Roho anatusaidia katika udhaifu wetu. Maana hatujui inavyotupasa kuomba; lakini Roho mwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa mlio wa huzuni usioelezeka.
Usikilize maneno yangu, ee Mwenyezi-Mungu, usikie ninavyopiga kite. Uwaadhibu kwa hatia yao ee Mungu; waanguke kwa njama zao wenyewe; wafukuze nje kwa sababu ya dhambi zao nyingi, kwa sababu wamekuasi wewe. Lakini wafurahi wote wanaokimbilia usalama kwako, waimbe kwa shangwe daima. Uwalinde wanaolipenda jina lako, wapate kushangilia kwa sababu yako. Maana wewe Mwenyezi-Mungu wawabariki waadilifu; wawakinga kwa fadhili zako kama kwa ngao. Usikilize kilio changu, Mfalme wangu na Mungu wangu, maana wewe ndiwe nikuombaye.
Asubuhi unioneshe fadhili zako, maana nimekuwekea tumaini langu. Unifundishe mwenendo wa kufuata, maana nakuelekezea ombi la moyo wangu.
Milima yaweza kutoweka, vilima vyaweza kuondolewa, lakini fadhili zangu hazitakuondoka, agano langu la amani halitaondolewa. Mimi Mwenyezi-Mungu nikuhurumiaye nimesema.
Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mkajifunze kwangu, maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtatulizwa rohoni mwenu. wamwulize: “Je, wewe ni yule anayekuja, au tumngoje mwingine?” Maana, nira niwapayo mimi ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”
Jinsi gani zilivyo bora fadhili zako! Wanadamu hukimbilia kivulini mwa mabawa yako. Wawashibisha kwa utajiri wa nyumba yako; wawanywesha kutoka mto wa wema wako. Wewe ndiwe asili ya uhai; kwa mwanga wako twaona mwanga.
Anayekaa chini ya ulinzi wa Mungu Mkuu, anayeishi chini ya kivuli cha Mungu Mwenye Nguvu,
Hasira yake hudumu kitambo kidogo, wema wake hudumu milele. Kilio chaweza kuwapo hata usiku, lakini asubuhi huja furaha.
Mungu ndiye mwenye kuniokoa, nitamtegemea yeye, wala sitaogopa; Mwenyezi-Mungu hunijalia nguvu; yeye mwenyewe ndiye aniokoaye.”
Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili, atainuka na kuwaonea huruma. Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki. Heri wote wale wanaomtumainia.
Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu, usikae mbali nami; ewe msaada wangu, uje haraka kunisaidia.
Mwenyezi-Mungu asifiwe siku kwa siku! Yeye hutubebea mizigo yetu; yeye ndiye Mungu wa wokovu wetu.
Heri mtu anayesaidiwa na Mungu wa Yakobo, mtu aliyeweka tumaini lake kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wake,
Basi, ndugu, kwa damu ya Yesu tunapewa moyo thabiti wa kuingia Mahali Patakatifu. Kama hao watu wanaomwabudu Mungu wangekuwa wametakaswa dhambi zao kweli, hawangejisikia tena kuwa na dhambi, na tambiko hizo zote zingekoma. Yeye ametufungulia njia mpya, njia ya uhai, kupitia lile pazia, yaani mwili wake mwenyewe. Basi, tunaye kuhani maarufu aliye na mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. Kwa hiyo tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu na imani timilifu, kwa mioyo iliyotakaswa kutokana na dhamiri mbaya, na kwa miili iliyosafishwa kwa maji safi.
Natazama juu milimani; msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu, aliyeumba mbingu na dunia.
Katika njia ya maamuzi yako tunakungojea ee Mwenyezi-Mungu; kulikumbuka jina lako ndiyo tamaa yetu.
Hata wanasimba hutindikiwa na kuona njaa; lakini wanaomtafuta Mwenyezi-Mungu hawakosi chochote chema.
Kutokana na hayo, tuseme nini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, nani awezaye kutupinga?
Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yakubalike mbele yako, ee Mwenyezi-Mungu, mwamba wangu na mkombozi wangu!
Lakini mimi nakuomba wewe, ee Mwenyezi-Mungu; nikubalie ombi langu wakati unaopenda, ee Mungu. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu. Wewe ni mkombozi wa kuaminika.
Namlilia Mungu kwa sauti, kwa sauti namlilia Mungu anisikie. Kisha nikasema, “Kinachonichoma zaidi ni kwamba, Mungu Mkuu hatendi tena kitu kwa ajili yetu!” Nitayakumbuka matendo yako, ee Mwenyezi-Mungu, naam, nitayafikiria maajabu yako ya hapo kale. Nitatafakari juu ya kazi zako, na kuwaza juu ya matendo yako makuu. Kila ufanyacho ee Mungu, ni kitakatifu. Ni mungu gani aliye mkuu kama Mungu wetu? Wewe ni Mungu unayetenda maajabu; wewe umeyaonesha mataifa uwezo wako. Kwa mkono wako wa nguvu uliwakomboa watu wako; uliwakomboa wazawa wa Yakobo na Yosefu. Maji yalipokuona, ee Mungu, maji yalipokuona, yaliogopa mno; naam, bahari ilitetemeka hata vilindini. Mawingu yalichuruzika maji, ngurumo zikavuma angani, mishale ya umeme ikaangaza kila upande. Kishindo cha ngurumo yako kilitokea katika kimbunga, umeme wako ukauangaza ulimwengu; dunia ikatikisika na kutetemeka. Wewe uliweka njia yako juu ya bahari; ulitembea juu ya maji yale mengi, lakini nyayo zako hazikuonekana. Wakati wa taabu namwomba Bwana; namnyoshea mikono yangu usiku bila kuchoka, lakini sipati faraja yoyote kwa mtu.
Fadhili zako ee Mwenyezi-Mungu zaenea hata mbinguni; uaminifu wako wafika mawinguni. Uadilifu wako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama vilindi vya bahari. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wawalinda wanadamu na wanyama
Basi, Mungu wangu, kwa utajiri wake mkuu kwa njia ya Kristo, atawapeni mahitaji yenu yote.
Jambo hili ni kwa wote, kwani hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi; Bwana wa wote ni mmoja, naye ni mkarimu sana kwao wote wamwombao.
Hata kabla hawajaniita, mimi nitawaitikia; kabla hawajamaliza kusema, nitakuwa nimewajibu.
Lakini wafurahi wote wanaokimbilia usalama kwako, waimbe kwa shangwe daima. Uwalinde wanaolipenda jina lako, wapate kushangilia kwa sababu yako.