Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 4:1 - Biblia Habari Njema

1 Ee Mungu mtetezi wa haki yangu, unijibu niombapo. Nilipokuwa katika shida, wewe ulinisaidia; unionee huruma na kusikia sala yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema - BHND

1 Ee Mungu mtetezi wa haki yangu, unijibu niombapo. Nilipokuwa katika shida, wewe ulinisaidia; unionee huruma na kusikia sala yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Ee Mungu mtetezi wa haki yangu, unijibu niombapo. Nilipokuwa katika shida, wewe ulinisaidia; unionee huruma na kusikia sala yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Nijibu nikuitapo, Ee Mungu wangu mwenye haki! Nipumzishe katika shida zangu; nirehemu, usikie ombi langu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Nijibu nikuitapo, Ee Mungu wangu mwenye haki! Nipumzishe katika shida zangu; nirehemu, usikie ombi langu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo; Uliniokoa nilipokuwa katika shida; Unifadhili na kuisikia sala yangu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

1 Ee Mungu mtetezi wa haki yangu, unijibu niombapo. Nilipokuwa katika shida, wewe ulinisaidia; unionee huruma na kusikia sala yangu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 4:1
35 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu alikuvuta akakutoa taabuni, akakuweka mahali pa wasaa pasipo shida, na mezani pako akakuandalia vinono.


Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu na apenda uadilifu; watu wanyofu watakaa pamoja naye.


Ee Mwenyezi-Mungu, mimi ni mtumishi wako; ni mtumishi wako, mtoto wa mjakazi wako; umenifungulia vifungo vyangu.


Mwenyezi-Mungu huwalinda wanyofu; nilipokuwa nimekandamizwa aliniokoa.


Unigeukie na kunionea huruma, kama uwatendeavyo wanaokupenda.


Usinitie hukumuni mimi mtumishi wako, maana hakuna yeyote aliye mwadilifu mbele yako.


Nakuita, ee Mungu, kwani wewe wanijibu; unitegee sikio, uyasikie maneno yangu.


Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Mbona uko mbali sana kunisaidia, mbali na maneno ya kilio changu?


Mtu huyo atapokea baraka kwa Mwenyezi-Mungu, na haki yake kwa Mungu mwokozi wake.


Unielekee, ee Mungu, unionee huruma, maana mimi ni mpweke na mnyonge.


Wewe hukuniacha nitiwe mikononi mwa maadui zangu; umenisimamisha mahali pa usalama.


Wewe umenitegemeza kwani natenda mema; waniweka mbele yako milele.


Kama paa atamanivyo maji ya kijito, ndivyo ninavyokutamani, ee Mungu wangu!


Moyo wangu umejaa mawazo mema: Namtungia mfalme shairi langu, ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.


Ee Mungu, unionee huruma, maana watu wananishambulia. Mchana kutwa maadui wananidhulumu.


Unihurumie, ee Mungu, unihurumie, maana kwako nakimbilia usalama. Kivulini mwa mabawa yako nitakimbilia usalama, hata hapo dhoruba ya maangamizi itakapopita.


Ee Mwenyezi-Mungu, usinikemee kwa hasira yako; usiniadhibu kwa ghadhabu yako.


Utuonee huruma, ee Mungu, utubariki; utuelekezee uso wako kwa wema;


Mungu anajulikana katika Yuda; jina lake ni kuu katika Israeli.


“Watasema juu yangu, ‘Haki na nguvu viko kwa Mwenyezi-Mungu peke yake.’” Wote waliomwakia hasira Mwenyezi-Mungu watamjia yeye na kuaibishwa.


Katika siku za utawala wake, Yuda ataokolewa na Israeli ataishi kwa usalama. Naye ataitwa, ‘Mwenyezi-Mungu ni uadilifu wetu.’


Bwana, Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu, huiimarisha miguu yangu kama ya paa, huniwezesha kupita juu milimani.


Mungu mwenyewe ndiye aliyewaunganisha nyinyi na Kristo Yesu. Mungu amemfanya Kristo awe hekima yetu; kwa njia yake sisi tunapatanishwa na Mungu, tunakuwa watu wake Mungu na kukombolewa.


Yeye alituokoa katika hatari kubwa ya kifo, na anaendelea kutuokoa; sisi tumemwekea tumaini letu kwamba atatuokoa tena,


Ndugu, tunataka kuwajulisheni taabu zilizotupata kule Asia; taabu hizo zilitulemea kupita kiasi, hata tukakata matumaini yote ya kuendelea kuishi.


Mwenyezi-Mungu ambaye ameniokoa makuchani mwa simba na dubu, ataniokoa kutoka kwa Mfilisti huyu.” Shauli akamwambia, “Nenda; naye Mwenyezi-Mungu awe pamoja nawe.”


Tufuate:

Matangazo


Matangazo